Israel yazuia Umoja wa Mataifa kuchunguza jinai zake za kivita Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80482-israel_yazuia_umoja_wa_mataifa_kuchunguza_jinai_zake_za_kivita_gaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekataa kushirikiana na timu ya Umoja wa Mataifa ambayo inachunguza jinai ilizozitenda katika vita vyake dhidi ya Ukanda wa Gaza mwaka jana.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Feb 18, 2022 03:14 UTC
  • Israel yazuia Umoja wa Mataifa kuchunguza jinai zake za kivita Gaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekataa kushirikiana na timu ya Umoja wa Mataifa ambayo inachunguza jinai ilizozitenda katika vita vyake dhidi ya Ukanda wa Gaza mwaka jana.

Meirav  Eilon Shahar, balozi wa utwala huo katika Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa mjini Geneva ametangaza msimamo huo katika barua ambayo binafsi amefikisha mbele ya Navi Pillay, mkuu wa Tume ya Uchunguzi wa jinai za kivita Gaza ambayo imeanzishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Eilon amedai kuwa utawala wa Israel hauamini kuwa haki itatendeka katika tume hiyo ambayo ameitaja kuwa eti ni njama ya kuiharibia jina Israel.

Mwezi Mei mwaka jana utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha vita dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kufuatia maandamano yaliyofanyika katika eneo hilo kuunga mkono Wapalestina wenzao wa Ukingo wa Magharibi ambao walikuwa wanakandamizwa kinyama na utawala huo ghasibu.

Hali baada ya hujuma ya Israel katika Ukanda wa Gaza

Katika vita hivyo vya siku 11, Wapalestina 248 waliuawa shahidi, wakiwemo watoto zaidi ya 60 huku wengine  1,200 wakijeruhiwa.

Vita hivyo vilikuwa vya nne vya pande zote vya utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo hilo ambalo liko chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala huo.

Kamishna wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa alitoa taarifa na kusema yamkini mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza yakawa ni  jinai za kivita.