Jeshi la Yemen ladhibiti eneo la kimkakati kusini magharibi mwa Ma'rib
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80852-jeshi_la_yemen_ladhibiti_eneo_la_kimkakati_kusini_magharibi_mwa_ma'rib
Vikosi vya jeshi la Yemen limefanya oparesheni katika mkoa wa Ma'rib na kufanikiwa kulidhibiti eneo la kistratejia katika mkoa huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2022 04:15 UTC
  • Jeshi la Yemen ladhibiti eneo la kimkakati kusini magharibi mwa Ma'rib

Vikosi vya jeshi la Yemen limefanya oparesheni katika mkoa wa Ma'rib na kufanikiwa kulidhibiti eneo la kistratejia katika mkoa huo.

Jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen yameendelea kusonga mbele katika maeneo mbalimbali nchini humo na kupelekea mamluki wa muungano wa Saudia na Imarati kurudi nyuma huko Ma'rib. Televisheni ya al Masira leo imeripoti kuwa, jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kulidhibiti eneo la al Saum huko kusini magharibi mwa Ma'rib.  

Vikosi vya Yemen vimetoa pigo kubwa kwa mamluki wa Saudi Arabia katika oparesheni hiyo. Kabla ya oparesheni hiyo, Brigedia Jenerali Yahya Saree msemaji wa rasmi wa jeshi la Yemen alibainisha kuwa, vikosi vya Yemen vitaendelea kufanya oparesheni hadi kukombolewa kikamilifu mkoa wa Ma'rib. 

Brigedia Jenerali, Yahya Saree 

Mapigano yanayoendelea huko Ma'rib ambayo yanahesabiwa kuwa oparesheni muhimu sana yanaweza kuainisha matokeo ya vita huko Yemen. Wanamuqawama wa Yemen wanazidi kupata mafanikio ya kimaidani huku upande wa pili ukiridhika pakubwa na mashambulizi ya anga ya wanajeshi vamizi wa Saudi Arabia na kujaribu kuvirudisha nyumba vikosi vya serikali ya Sana'a kwa kustafidi  na mashambulizi hayo tajwa.

Mkoa wa Ma'rib katika siku za karibuni umekumbwa na mashambulizi mengi ya anga ikilinganishwa na miezi kadhaa iliyopita.