Kudhihirika zaidi kutokuwa na natija vikwazo vya Marekani ulimwenguni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i98728-kudhihirika_zaidi_kutokuwa_na_natija_vikwazo_vya_marekani_ulimwenguni
Mkutano wa kibiashara wa mataifa ya Kiarabu na China umefanyika katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh katika hali ambayo, Beijing inafanya juhudi za kuhakikisha kuwa inanyakua nafasi ya kwanza ya biashara katika eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2023 07:45 UTC
  • Kudhihirika zaidi kutokuwa na natija vikwazo vya Marekani ulimwenguni

Mkutano wa kibiashara wa mataifa ya Kiarabu na China umefanyika katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh katika hali ambayo, Beijing inafanya juhudi za kuhakikisha kuwa inanyakua nafasi ya kwanza ya biashara katika eneo la Asia Magharibi.

Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana mkutano wa kibiashara wa mataifa ya Kiarabu na China linahesabiwa kuwa tukio kubwa na la aina yake la kiuchumi la China na mataifa ya Kiarabu. Hii ina maana kwamba, mataifa ya Kiarabu yamo mbioni kubadilisha utendaji wao kutoka upande wa Magharibi na hususan Marekani na kuelekea upande wa Mashariki na ndio maana yanafanya juhudi za kuvutia ushirikiano na uwekezaji na taifa la China.

Hata hivyo, suala hili halifuatiliwi tu na nchi za Kiarabu, kwa sababu kulingana na ripoti za habari, China ni mshirika wa kwanza wa biashara wa nchi tisini duniani.

Watalaamu wa masuala ya kimataifa wanasema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni China imeonyesha kuwa iko tayari kuwekeza katika nchi mbalimbali na hivi sasa nchi za bara la Asia hususan nchi za Kiarabu zinajaribu kuongeza ushirikiano na China kutokana na kutumia nyanja mbalimbali, ili kupanua ushirikiano wa kibiashara.

Katika mkutano wa Waarabu na China mjini Riyadh, kumechunguzwa njia za kupata ustawi na maendeleo endelevu. Kwa mtazamo huo inaonekana kwamba msingi wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili unazingatia data. Kwa sababu ukuaji na maendeleo katika kila sekta yanatokana na takwimu.

 

China ndiyo mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi za Kiarabu ikiwa na mabadilishano ya biashara ya dola bilioni 430 mwaka 2022, na kasi ya ukuaji wa biashara kati ya pande hizo mbili ilikuwa 31% ikilinganishwa na mwaka uliopita. Hata hivyo, inaonekana kuwa nchi za Kiarabu zinatarajia kupanua kiwango cha uhusiano wao na China katika sekta kama vile teknolojia, nishati mbadala, kilimo, ili ziweze kutumia teknolojia ya kisasa zaidi duniani.

Ridha Abdul-Salam, mweledi na mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema kuhusiana na hili kwamba:

Kutiwa saini kwa mkataba wa dola bilioni kumi kati ya nchi za Kiarabu na China katika siku ya kwanza ya mkutano wa pande hizo mbili huko Riyadh kunaonyesha kuwa, kuna maendeleo muhimu sana katika uhusiano wa Kiarabu na China. Wakati huo huo, Marekani ilijaribu kuizingira China na kuidhoofisha kwa kuanzisha vita vya kibiashara na China na kuweka vikwazo mbalimbali dhidi yake. Lakini mafanikio ya China katika nyanja za kibiashara yanaonyesha kushindwa na kufeli Marekani kuhusiana na hili.

Hapana shaka kuwa, kupelekwa mafuta ya Russia nchini Pakistan huku Marekani ikiwa imeweka vikwazo mbalimbali dhidi ya Moscow kunaonyesha kutofaulu kwa vikwazo vya Washington dhidi ya mataifa mbalimbali.

Mkutano wa kibiashara wa China na mataifa ya Kiarabu mjini Riyadh Saudi Arabia

 

Aidha, nchi na mataifa tofauti hushirikiana kwa kuzingatia maslahi yao, na matarajio ya Marekani kwamba nchi huru na zisizokubali kuburuzwa zitafuata sera za Washington si ya mahala pake kabisa. Kwa hivyo, kuwasili shehena ya kwanza ya meli ya mafuta ya Russia na kutia nanga katika bandari ya Karachi ya Pakistan kunaweza kutathminiwa katika fremu hii.  Kwa hivyo, kinyume na mtazamo wa madola ya Magharibi, vikwazo dhidi ya Russia havikuweza kulitenga taifa hilo kama ilivyokuwa ikitarajia Washington. Baada ya vita vya Ukraine, nchi za Magharibi hasa Marekani zilikusudia kuzidisha kampeni na propaganda zao dhidi ya Russia kwa kuzidisha vikwazo dhidi ya Moscow, lakini zimeshindwa kufikia malengo yao.

Vyovyote iwavyo, utendaji wa nchi za Kiarabu wa kutaka kupanua ushirikiano na China unaonyesha kuwa, nchi za Kiarabu ambazo kijadi ziliungana na kuwa pamoja na Marekani zimeipuuza Washington na filihali zimezinduka na kuamua kufanya maamuzi kwa mujibu wa maslahi ya wananchi wao, jambo ambalo linahesabiwa kuwa ni kushindwa pakubwa Marekani katika ulimwengu wa Kiarabu.