-
UNICEF: Mamilioni ya watoto wanakabiliwa na hatari ya utapiamlo nchini Yemen
Mar 24, 2023 22:50Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeonya kuwa mamilioni ya watoto wanakabiliwa na hatari ya utapiamlo nchini Yemen ikiwa fedha hazitatolewa haraka kwa nchi hiyo ya Kiarabu iliyokumbwa na vita, ambapo mtoto mmoja hufariki dunia kila baada ya dakika kumi.
-
Baada ya kupita miaka kumi, Saudia na Syria zinatarajia kufungua tena balozi zao
Mar 24, 2023 06:31Televisheni ya Saudi Arabia imemnukuu afisa mmoja katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo na kutangaza kuwa Riyadh imeanza mazungumzo na Syria ili kuanza tena kutoa huduma za kibalozi.
-
Waziri Mkuu wa Lebanon: Kuna ulazima wa kuchukua hatua haraka ili kuiokoa nchi
Mar 24, 2023 06:30Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Miqati amesema, kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuiokoa nchi hiyo.
-
Maafisa wa Iran, Lebanon wazungumzia matukio ya kieneo mjini Beirut
Mar 24, 2023 04:21Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Mahusiano ya Kigeni la Iran, Kamal Kharrazi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah mjini Beirut, ambapo wamejadili matukio ya hivi sasa ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Asia Magharibi.
-
Uamuzi madhubuti wa bunge la Jordan wa kumfukuza balozi wa Israel.
Mar 24, 2023 03:45Mvutano umeibuka katika uhusiano wa Amman na Tel Aviv kufuatia uamuzi imara wa Bunge la Jordan wa kumfukuza balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo.
-
Marubani wa Israel wakataa kumpeleka Netanyahu Uingereza
Mar 24, 2023 03:35Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amelazimika kuakhirisha safari yake ya kuitembelea Uingereza, baada ya marubani kadhaa wa utawala huo kukataa kumsafirisha kwa ndege katika nchi hiyo ya Ulaya mtawala huyo mwenye misimamo mikali.
-
Ubaguzi wa rangi wa baraza la mawaziri la Netanyahu na hasira ya serikali ya Jordan
Mar 23, 2023 22:50Matamshi ya karibuni ya mmoja wa mawaziri wa baraza lenye misimamo ya kupindukia mipaka la Benhamini Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel yameikasirisha serikali ya Jordan. Misimamo mikali na ya ubaguzi wa rangi ya baraza hilo hadi sasa imeugharimu pakubwa utawala huo kieneo na kimataifa.
-
GCC: Mapatano ya Saudia, Iran kuhitimisha migogoro katika eneo
Mar 23, 2023 07:41Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC) limepongeza makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Saudi Arabia ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia uliokuwa umevunjika kwa kipindi cha miaka saba.
-
Nasrullah: Uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Lebanon utajibiwa haraka
Mar 23, 2023 07:33Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amepuuzilia mbali vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na maafisa wa utawala haramu wa Israel vya kuwepo uwezekano wa kuivamia kijeshi Lebanon na kusisitiza kuwa, uchokozi wowote wa Israel dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu utapata jibu la haraka.
-
Kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kusini mwa Quds Tukufu
Mar 23, 2023 04:33Meya wa mji mtakatifu wa Quds ametoa idhini ya kujengwa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika mji huo, jambo ambalo linaenda kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.