-
Ripoti ya kushtusha ya Umoja wa Mataifa; mauaji ya kimbari ya Wapalestina Ghaza yangali yanaendelea
Nov 06, 2025 23:17Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza yangali yanaendelea.
-
Hizbullah: Hatutaki mazungumzo na Israel, hatutaki makubaliano nao
Nov 06, 2025 23:06Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeandika barua ya wazi kuhusu mitego iliyowekwa na Wazayuni kupitia kile kinachodaiwa ni mazungumzo ya amani na kusema kuwa, lengo la mazungumzo hayo ni kulitwisha taifa la Lebanon siasa za upande mmoja za Israel na kuvunja nguvu mwamko wa wananchi wa Lebanon wa kupigania haki zao mbele ya adui mpenda vita. Imesema: Mapambano ndiyo yanayolifanya taifa kubaki kuwa na heshima.
-
Takriban watu 90 wamefariki dunia baada ya kimbunga cha Kalmaegi kuiathiri Ufilipino
Nov 06, 2025 07:40Watu wasiopungua 90 wamefariki dunia na wengine 75 hawajulikani walipo hadi sasa kufuatia kimbunga cha Kalmaegi kuathiri maeneo ya kati ya Ufilipino jana Jumatano.
-
Google yafuta ushahidi wa video za uhalifu wa Israel huko Palestina
Nov 06, 2025 07:38Nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kwamba kampuni ya Kimarekani ya Google imefuta zaidi ya video 700 zinazoonyesha uhalifu wa kivita wa utawala wa Israel kutoka kwenye mtandao wa intaneti.
-
Gharibabadi: Uhusiano imara wa Iran na Saudi Arabia utaleta manufaa makubwa
Nov 06, 2025 04:21Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kimataifa na kisheria, Kazem Gharibabadi, amesisitiza umuhimu wa kistratejia wa kurejeshwa kwa uhusiano na Saudi Arabia, akisema kuwa kuimarika kwa mahusiano ya kirafiki kati ya Tehran na Riyadh ni kwa faida za pande mbili na pia ni nguvu muhimu ya kuimarisha uthabiti wa eneo na amani ya kimataifa.
-
Kwa nini kilio cha machungu ya Wapalestina hakisikiwi na walimwengu?
Nov 06, 2025 00:34Hakuna usiku mtulivu huko Gaza, si kabla ya kusitishwa kwa mapigano au baada ya tangazo la amani na usiitishaji vita la Sharm el-Sheikh nchini Misri.
-
Reuters: Serikali ya Trump inafikiria kuizuia Saudia ndege za kisasa za kivita za F-35
Nov 05, 2025 23:49Shirika la habari la Reuters limenukuu chanzo cha kuaminika ambacho hakikutaka kitajwe na kutangaza kwamba serikali ya Trump inapitia ombi la Saudi Arabia la kununua ndege 48 za kivita za kisasa za F-35, mpango wa mabilioni ya dola ambao umeondoa moja ya vikwazo vikubwa katika Wizara ya Vita ya Marekani na ambao unajadiliwa sanjari na ziara ijayo ya Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman huko nchini Marekani.
-
Hamas yapinga kutumwa jeshi la kigeni Gaza mbadala wa jeshi vamizi la Israel
Nov 05, 2025 03:39Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza imesema kuwa haiwezakani kutumwa kikosi cha kijeshi cha kigeni katika eneo hilo ambacho kitahudumu kama mbadala wa jeshi vamizi la Israel.
-
Yemen: Tumejiandaa kwa vita vikubwa na Israel
Nov 04, 2025 23:47Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, harakati za Muqawamaa zimejiandaa kwa ajili ya awamu ijayo ya mapambano na utawala wa Kizayuni wa Israel, kwani zinaamini kwamba eneo hili halitakuwa imara kwa muda mrefu maadamu Palestina inaendelea kukaliwa kwa maabavu na dola pandikizi la Kizayuni ambalo muda wote linapanga njama dhidi ya Waislamu.
-
Utafiti: Vita vya mauaji ya kimbari vya Israel vimegharimu zaidi ya miaka milioni 3 ya maisha ya mwanadamu huko Gaza
Nov 04, 2025 23:36Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la Lancet umefichua kuwa zaidi ya miaka milioni tatu ya maisha ya binadamu yamepotea katika Ukanda wa Gaza tangu utawala ghasibu wa Israel uanzishe kampeni yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro, mwezi Oktoba mwaka 2023.