Wasweden wavunjia tena heshima Qur'ani Tukufu kwa himaya ya polisi
Kundi la wabaguzi wa rangi na wenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Denmark limechoma moto tena nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya balozi za Uturuki na Iraq nchini humo.
Ripoti ya shirika la habari la Anatoly imesema, wanachama wa kundi linalojiita Wazalendo wa Denmark wamechoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya ubalozi wa Uturuki. Wanachama wa kundi hilo pia wamechoma moto nakala nyingine ya Qur'ani mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Copenhagen.
Wanachama wa kundi hilo walishikilia mabango na kutoa nara dhidi ya Uislamu na baadaye kusambaza picha na video za vitendo hivyo viovu katika mitandao ya kijamii.
Vitendo hivi vya kichochezi vimefanyika chini ya usaidizi na himaya ya polisi wa Denmark.
Dharau na vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Sweden na Denmark vimeongezeka sana katika wiki za hivi karibuni, na vimekabiliwa na malalamiko katika nchi za Waislamu na kwenye duru za kimataifa.
Nchi za Magharibi zinaruhusu kutukana na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu, hasa kuchoma moto Qur'ani Tukufu kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.
Mwezi uliopita wa Julai Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano liliidhinisha azimio lililopendekezwa na nchi za Kiislamu la kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu jambo hilo pamoja na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kutakiwa kutoa ripoti kuhusu suala hilo.