Oct 14, 2023 13:36 UTC
  • Ujerumani yapiga marufuku kuvaa skafu za Palestina maskulini

Viongozi wa Ujerumani wamepiga marufuku rasmi kuvaa leso na skafu za Palestina maskulini ikiwa ni kuendelea kuunga mkono waziwazi jinai na mauaji ya watoto wadogo na wanawake wa Palestina yanafanywa hivi sasa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Jumamosi iliyopita ya tarehe 7 Oktoba, 2023, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS iliendesha opereseheni ya kishujaa na ya kihistoria ya #Kimbunga_cha_al-Aqsa kwa kushambulia kwa makombora maeneo mbalimbali ya utawala wa Kizayuni ukiwemo mji mkuu Tel Aviv na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya Ashdod na Asqalan. 

Mbali na kuyateka kwa muda baadhi ya maeneo na kambi za kijeshi za Wazayuni, wanamapambano hao wa Palestina waliyapiga kwa mamia ya makombora na maroketi maeneo tofauti ya utawala wa Kizayuni.

Baada ya matukio hayo, madola ya Magharibi yamezidi kuonesha undumilakuwili wao katika masuala mbalimbali yakiwemo ya uhuru wa kusema, kuamini na kuvaa mtu anachopenda. Aidha yamekuwa yakiunga mkono waziwazi jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wanawake, watoto na wananchi wa kawaida wa Palestina. 

Wazayuni watakwenda kujibu kila jinai waliyoifanya dhidi ya watoto wasio na hatia

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, maafisa wa elimu wa Ujerumani wametoa amri kwa wakuu wa skuli za nchi hiyo kupiga marufuku harakati zozote za watu kutangaza imani zao ambazo zinahusiana na kuwaunga mkono Wapalestina na muqawama wa Kiislamu hususan harakati za HAMAS ya Palestina na Hizbullah ya Lebanon.

Afisa huyo wa serikali ya Ujerumani ameongeza kuwa, mbali na kupigwa marufuku skafu za Palestina kuvaliwa maskulini, Ujerumani imepiga marufuku pia matamshi, vitendo na nembo yoyote inayounga mkono mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni. 

Wapigania haki na uhuru duniani wanailaumu serikali ya Ujerumani kwa hatua zake hizo ambazo zinakinzana moja kwa moja na haki za kimsingi za raia wa nchi hiyo.

Tags