Oct 17, 2023 13:41 UTC
  • Russia: Kustawisha uhusiano wa kimkakati na China ni kipaumbele chetu cha kipekee

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa kustawisha uhusiano wa kimkakati na China ni kipaumbele cha kipekee kwa Moscow, na akauelezea uhusiano wa Moscow na Beijing kuwa ni kama mfano wa ushirikiano wa kiserikali kati ya madola makubwa yenye nguvu katika karne ya 21.

Kwa mujibu wa IRNA, Maria Zakharova amesisitiza kwamba ziara ya Rais Vladimir Putin wa Russia nchini China itakuwa moja ya matukio muhimu katika uhusiano wa pande mbili.
 
Zakharova amebainisha kuwa viongozi wa Russia na China wanalipa umuhimu mkubwa suala la kustawisha mtawalia uhusiano wa nchi mbili, na akaongeza kuwa mawasiliano yoyote yanayofanywa kati ya viongozi wakuu wa nchi hizo huwa ni fursa mwafaka ya kujadidisha misimamo na kukubaliana juu ya utekelezaji wa mipango mikubwa.
 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amezungumzia makubaliano yaliyofikiwa ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Russia na kuidhinishwa kwa ramani ya njia ya Beijing-Eurasia na akabainisha kwamba, ramani hiyo ya njia inaandaa mazingira mwafaka katika mwenendo wa kustawisha miradi ya pamoja ya viwanda.
Rais Vladimir Putin wa Russia (kushoto) na Rais Xi Jinping wa China

Maria Zakharova ameashiria pia mpango wa kimkakati wa Moscow wa  "Kuunganisha Ulaya na Asia" na kueleza kuwa Russia inaona mpango huo muhimu kama msingi na kipengele muhimu katika kuunda mfumo jumuishi wa kupanua mashirikiano ya Eurasia.

 
Rais Vladimir Putin wa Russia amewasili Beijing kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Xi Jinping wa China pamoja na kushiriki katika mkutano wa tatu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".
 
Rais wa Russia ameonyesha hamu ya kushirikiana na mpango wa China wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kwa sababu hiyo, alishiriki pia katika mikutano iliyopita ya mpango huo.../

 

Tags