Venezuela yaalani kitendo cha Marekani cha kuiba ndege yake
(last modified Tue, 13 Feb 2024 11:51:36 GMT )
Feb 13, 2024 11:51 UTC
  • Venezuela yaalani kitendo cha Marekani cha kuiba ndege yake

Serikali ya Venezuela imelaani vikali kitendo cha Marekani cha kuiba waziwazi ndege iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni moja la Venezuela.

Ndege hiyo aina ya Boeing 300-747 mali ya kampuni ya Emtrasur ya Venezuela ambayo imewekewa vikwazo na Wizara ya Fedha ya Marekani, ilikamatwa na kutwaliwa nchini Argentina Juni 2022 licha ya ukweli kwamba,  hakuna ushahidi wa kufanyika kitendo chochote kinyume na sheria na wafanyakazi au kuhusu shehena ya mizigo iliyokuwa imeibeba wakati ilipozuiliwa. 

Ndege ya Kampuni ya Venezuela ya Emtrasur 

Taarifa ya Wizara ya Sheria ya Marekani inasema: Ndege hiyo ya Venezuela ilikuwa imefika katika jimbo la Florida na kwamba  itaendelea kushikiliwa.  

Serikali ya Venezuela imelaani wizi huo wa waziwazi wa ndege ya nchi hiyo na kutangaza kuwa, wizi wa ndege hiyo mali ya Kampuni ya Emtrasur ulifanyika kwa njama ya serikali za Marekani na Argentina, na kuitaja hatua hiyo kuwa ni wizi wa kufedhehesha. 

Serikali ya Venezuela pia imesema: Marekani na Argentina zimekiuka sheria zote za usafiri wa anga pamoja na haki za kibiashara, kiraia na kisiasa za kampuni iliyotajwa na zimehatarisha usalama wa usafiri wa anga katika eneo hilo.  

Katika taarifa yake, Shirikisho la Bolivia la Mataifa ya Amerika Kusini (ALBA) pia limetaja kitendo cha  Marekani  kuiba waziwazi ndege ya Venezuela kuwa ni ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Venezuela. 

Tags