Feb 22, 2024 11:32 UTC
  • Wananchi wa Ulaya wakata tamaa, hawatarajii kupata ushindi Ukraine

Matokeo ya uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni yanaonesha kuwa, ni asilimia 10 tu ya wananchi wa nchi za Ulaya wanaoamini kwamba Ukraine inaweza kushinda kwenye vita vyake na Russia.

Kesho Jumamosi, tarehe 24 Februari utaingia mwaka wa pili wa tangu kuanza vita vya Ukraine na Russia. Vita hivyo vilianza tarehe 24 Februari, 2022 na hadi hivi sasa makumi ya mabilioni ya dola za Kimarekani yameshatumika kwa sura ya misaada ya kijeshi, kisiasa, kipropaganda na kila kila kitu kutoka nchi za Ulaya na Marekani kwa ajili ya serikali ya Ukraine dhidi ya Russia.

Pamoja na nchi za Ulaya na Marekani kujiingiza kwenye hasara kubwa kiasi chote hicho kwenye vita vya Ukraina lakini hazijaambulia chochote isipokuwa kuuawa makumi ya maelfu ya watu hasa wa Ukraine, mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi na kuchakazwa na kusambaratishwa vibaya miji na miundombinu ya Ukraine.

 

Kupata vipigo vya mfululizo Ukraine kwenye medani za vita kumewakatisha tamaa wananchi za nchi za Magharibi ambao hivi sasa ni asilimia 10 tu wanaoamini kuwa Ukraine inaweza kushinda vita hivyo. Hiyo asilimia 10 ni ya wale watu wa Ulaya wenye taasubu kubwa ambao wanajiona wao ndio bora kuliko mwanadamu mwingine yeyote.

Televisheni ya Russia Today imenukuu matokeo ya maoni yaliyofanywa na Baraza la Uhusiano wa Kigeni la Ulaya (ECFR) yakionesha kuwa, asilimia kubwa ya wananchi wa nchi za Ulaya na Marekani wanaamini kwamba, vita vya Ukraine vitamalizika kwa mazungumzo na hawana matumaini kabisa ya kuweza Ukraine kushinda vita hivyo.

Kadiri siku zinavyopita ndivyo safu za jeshi la Ukraine linavyozidi kusambaratishwa na kupoteza vituo muhimu. Wiki chache tu nyuma jeshi la Russia liliteka ngombe kubwa ya nchi za Magharibi ya Avdiivka na kutoa pigo kubwa kwa waungaji mkono wa serikali ya Kyiv.

Tags