Apr 11, 2024 02:21 UTC
  • Juhudi mpya za kuushtaki utawala wa Kizayuni wa Israel

Huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukuendeleza jinai dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Gaza, nchi nyingi za dunia zinajaribu kusimamisha vita vya Gaza na kuufikisha kizimbani utawala wa kutokana na jinai zake za mauaji ya kimbari. Jitihada hizo hasa zimeonekana kushika kasi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Kuhusiana na hilo,  Nicaragua kumefanyika kikao a kwanza cha Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini The Hague, kilichofanyika kuchunguza kesi ya malalamiko ya nchi hii dhidi ya Ujerumani.

Nicaragua imeitaka mahakama kutoa maagizo ya awali yanayojulikana kama hatua za muda, ikiwa ni pamoja na kwamba Ujerumani inapaswa kusitisha "mara moja"  msaada wake kwa Israel, haswa, msaada wake wa kijeshi hasa kutokana na kuwa msaada huo unaweza kutumika katika ukiukaji wa Mkataba wa Mauaji ya Kimbari na sheria za kimataifa.

Timu ya wanasheria wa Nicaragua katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ilieleza kuwa mahakama hii inapaswa kuiamuru Ujerumani kuacha kuunga mkono uharibifu wa Palestina na mauaji ya halaiki ya Wapalestina na kuongeza: Taifa la Palestina linakabiliwa na hali mbaya za zaidi ya  uharibifu za kijeshi katika historia ya kisasa, na Ujerumani kwa kuiunga mkono Israel, inawajibika na ni mshirika katika mauaji ya kimbari huko Gaza na hivyo imekiuka mkataba wa kuzuia mauaji ya kimbari.

Mawakili wa Nicaragua wamesema: Kampuni za silaha za Ujerumani zimenufaika pakubwa na vita dhidi ya Gaza. Katika malalamiko yake, Nicaragua imesema kuwa ni "lazima na udharura" kwa mahakama hiyo kuamuru kutekelezwa kwa hatua za kuzuia uuzaji wa silaha kwa Israel kwa kuzingatia hatari kwa maisha ya mamia kwa maelfu ya watu wa Palestina.

Hivi karibuni Afrika Kusini nayo pia ililalamikia rasmi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya Israel kwa uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari ya Wapalestina huko Gaza.

Baada ya malalamiko ya Afrika Kusini, nchi nyingi zimeunga mkono malalamiko hayo na kutaka kuchunguza mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina  huko Gaza.

Ujumbe wa mawakili wa Afrika Kusini katika kikao cha Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu jinai za mauaji ya kimbari za Israel dhidi ya Gaza

Ijapokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ilitoa wito wa kusitishwa operesheni za kijeshi za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina, lakini waitifaki wa Israel ikiwemo Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya hususan Ujerumani wanaendelea kuzuwia kumalizika vita hivyo au kusimamisha jinai za utawala huo ghasibu kwa kutoa msaada wa kijeshi na silaha kwa utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Uchumi ya Ujerumani, nchi hiyo ilikuwa muuzaji mkubwa wa silaha kwa Israel mwaka 2023.

Ujerumani na Marekani zinasambaza takriban asilimia 99 ya silaha zote zinazoingizwa nchini Israel; hayo ni kulingana na uchambuzi uliochapishwa Machi na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI).

Kwa msingi hiyo Mamia ya watumishi wa umma wa Ujerumani wameungana na harakati ya kumtaka Kansela Olaf Scholz aache kuupatia utawala haramu wa Israel huku utawala huo ukiendelea na jinai zake za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Takriban wafanyikazi waandamizi 600 wa sekta ya umma walimwandikia barua Scholz siku ya Jumatatu, wakimtaka yeye na maafisa wake wakuu "kukomesha ufikishaji wa silaha kwa Israeli mara moja."

Katika suala hili, katika hatua mpya, wabunge 16 zaidi wa Marekani wamemuandikia barua  Rais Joe Biden na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken, wakiomba kusitisha uhamisho wa silaha kwa Israel.
Kufikia sasa, idadi ya wapinzani wa mauzo ya silaha kwa Tel Aviv katika Congress imefikia 56.

Francesca Albanese, ripota maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Palestina, amesema katika ripoti yake ya hivi punde kuhusu mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa Gaza yanayotekelezwa na jeshi la Israel kwamba: "Jinai ambazo Israel imetenda huko Gaza tangu Oktoba 7 zinaweza kuichukua Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) miaka hamsini kusikiliza kesi hiyo kwa kuzingatia kasi ya sasa ya mahakama hiyo.

Inaonekana kwamba ukubwa wa jinai za Israel umesababisha maoni ya wananchi katika nchi nyingi kutaka taasisi za kimataifa kuchukua hatua za haraka kusitisha mauaji ya Wapalestina sambamba na kuufikisha kizimbani utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake za mauaji ya kimbari. Matakwa hayo ya dunia yamepelekea utawala wa Israel na waitifaki wake wazidi kutengwa zaidi duniani.