May 08, 2024 02:24 UTC
  • HRW yaikosoa Marekani kwa kuupa silaha utawala wa Kizayuni

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limetangaza katika ripoti yake kuwa Israel imetumia silaha kutoka Marekani katika mashambulizi yake dhidi ya eneo la al Habariyeh huko Lebanon.

Jeshi la utawala wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari huko Gaza, Machi 27 mwaka huu lilitumia silaha za mashambulizi ya pamoja (JDAM) kutoka Marekani na bomu lililokuwa na uzito wa karibu kilo 230 lililoundwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kushambulia jengo moja la kiraia katika eneo la Hebariyeh kusini mwa Lebanon. Wafanyakazi saba wa misaada ya kibinadamu wa kujitolea waliuawa katika hujuma hiyo ya Israel. 

Shambulio la kigaidi la Israel katika jengo la misaada ya kibinadamu, Lebanon 

Shirika la Habari la Iran (IRNA) jana liliripoti kuwa, shirika la Human Rights Watch limelitaja shambulizi la utawala wa Israel katika kituo cha huduma za kibinadamu huko kusini mwa Lebanon kuwa ni kinyume cha sheria na dhidi ya raia, na kusisitiza kuwa hujuma hiyo ni jinai ya kivita. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon pia imewasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) huko Hague na kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu jinai hiyo ya utawala wa Israel dhidi ya kituo cha misaada ya kibinadamu katika eneo la Hebariyeh, Lebanon. 

Utawala wa Kizayuni umefanya shambulio hilo kusini mwa Lebanon katika hali ambayo Tel Aviv iliihakikishia Marekani kwamba haitatumia silaha ilizopewa na Washington kinyume cha sheria. 

Tags