Aug 04, 2024 03:00 UTC
  • Maandamano ya kuiunga mkono Palestina yafanyika katika nchi 6 za Ulaya

Maandamano makubwa ya kuiunga mkono na kutangaza mshikamano na Palestina yameshuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi barani Ulaya.

Shirika la habari la hapa nchini la Mehr limeripoti kuwa, miji mikuu  na mikubwa duniani ilishuhudia maandamano makubwa jana Jumamosi ambapo wakazi wa miji hiyo wametaka kusitishwa mara moja hujuma na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

Maelfu ya wakazi katika miji mbalimbali ikiwemo Manchester na London nchini Uingereza jana walimiminika katika mitaa mbalimbali ya miji hiyo kuwaunga mkono raia wa Palestina. 

Maandamano ya kuiunga mkono Palestina mjini London

Wakazi katika miji ya Aarhus na Copenhagen nchini Denmark, Rotterdam na Amsterdam huko Uholanzi, Uppsala, Malmö na Helsingborg nchini Uswidi, Stuttgart nchini Ujerumani, Paris, nchini Ufaransa jana waliandamana kuonyesha mshikamano na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. 

Waandamanaji hao wametaka kusimamishwa vita na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza haraka iwezekanavyo, kutumwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo na kukomeshwa vigezo vya undumakuwili mkabala wa radimali na hatua za kimataifa kuhusu vita vya Gaza.  

 

Tags