Umoja wa Mataifa: Mataifa 22 yanakabiliwa na hatari ya njaa duniani
Umoja wa Mataifa umetangaza kuuwa, ghasia, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na changamoto za kiuchumi zimepelekea njaa na wakati mwingine hali ya ukame kwa mataifa 22, bila kuweko dalili za hali kuimarika ndani ya miezi 6 ijayo.
Arif Husain, ambaye ni mchumi mkuu kwenye Shirika la Chakula Duniani WFP, amesema, hali ni mbaya zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, Sudan, Sudan Kusini, Haiti na Mali, ambako mamilioni ya watu wapo kwenye hatari zaidi ya ukosefu wa usalama wa chakula, ikiwa na maana kwamba hali ya njaa kuu inashuhudiwa.
Huko Gaza Palestina, mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yameonya kuhusu kudorora kwa hali katika miezi ya karibuni. Hali hiyo imechochewa zaidi na huujuma na mashambulio ya Israel dhidi ya Ukanda huo ambayo yamehatarisha upelekaji misaada ya kibinadamu pamoja misaada mingine kwa Wapalestina waliokwama kwenye vita hivyo.
Husain ameongeza kusema kuwa asilimia 91 ya wakazi wa Gaza wapo kwenye baa la njaa, takriban 345,000 miongoni mwao wakikabiliwa na hali zinazofanana na ukame. Hali ya Sudan ni mbaya zaidi kutokana na kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa ni kubwa zaidi.