Demokrasia ya BBC; "Uhuru wa kujieleza" ni kwa wapinzani wa Iran tu!
-
Gary Lineker
Gary Lineker, mtangazaji mashuhuri na maarufu wa BBC, amefutwa kazi na shirika hilo baada ya miaka 26 ya utumishi kwa sababu tu ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.
Kufutwa kazi mtangazaji maarufu wa BBC, Gary Lineker, kwa mara nyingine tena kumefichua uwongo mkubwa wa "uhuru wa kujieleza" katika nchi za Magharibi ambazo zinaruhusu tu maneno yanayooana na sera za ubeberu wa kimataifa na kukandamiza sauti yoyote pinzani.
Gary Lineker, ambaye kwa miaka mingi alikuwa mtu maarufu asiye na upendeleo katika vipindi vya michezo vya BBC, aliandamwa baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X akiunga mkono watu wa Palestina. Aliandika kwenye mtandao wa X kwamba: "Watoto wasio na hatia wa Gaza ni wahanga wa sera za ukatili za Israel." Baada ya kutuma ujumbe huo, BBC ilimtuhumu kuwa ana "chuki dhidi ya Wayahudi" na ikamlazimisha kujiuzulu.
Kampeni ya Mshikamano na Palestina imeutaja uamuzi wa BBC wa kumtimua Gary Lineker kuwa 'wakati wa aibu kwa shirika la utangazaji linalofadhiliwa na umma'.
Baraza la Waislamu la Uingereza pia limemshukuru Lineker kwa 'kupaza sauti kwa ajili ya wasio na sauti'.
Kesi hii ya nguli wa vipindi vya michezo na hasa Match of the Day vya BBC, Gary Lineker inaakisi tena sera za kinafiki na undumakuwili za Uingereza na Magharibi kwa ujumla kuhusu suala la uhuru wa kusema na kujieleza.

Kwa Wamagharibi, iwapo mtu yeyote atakosoa mauaji yanayofanywa na Saudi Arabia (mshirika wa Magharibi), dhidi ya watoto wa Yemen anaitwa "gaidi", na akilaani mauaji ya yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza, wanaitwa "anti-Semite" au mwenye chuki dhidi ya Wayahudi. Wakati huo huo iwapo atakariri uongo dhidi ya Iran, anakuwa "mwandishi huru wa habari" na kupewa tuzo!