Zarif awasili nchini Nicaragua
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewasili Managua mji mkuu wa Nicaragua katika safari yake ya pili katika ziara yake ya kiduru katika nchi sita za Amerika ya Latini.
Muhammad Javad Zarif ambaye juzi alasiri katika safari yake ya kwanza aliwasili Havana mji mkuu wa Cuba, jana alikutana na viongozi wa Cuba ambapo walibadilishana mawazo kuhusu kuongezeka uhusiano wa pande mbili na pia walichunguza nyanja mbalimbali za ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tehran na Havana.
Zarif pia alihudhuria katika eneo la kumbukumbu ya Jose Martin shujaa wa uhuru wa Cuba na akaweka shada la mauaji katika kumuenzi shujaa huyo mpigania uhuru. Baadaye Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alifanya mazungumzo na Rodrigo Malmierca Waziri wa Biashara ya Nje wa Cuba na kuchunguza vipengee mbalimbali vya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi mbili.
Zarif pia alishiriki kwenye hafla ya ufunguzi wa kikao cha kwanza cha kibiashara kati ya Iran na Cuba na akahutubia kwenye hafla hiyo na kisha akafanya mazungumzo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Waziri mwenzake wa nchi hiyo Rodriguez Pereira kuhusu uhusiano wa pande mbili.
