Barret: Polisi ya Marekani imejifunza ukatili kutoka Israel
Mchanganuzi wa masuala ya siasa na mwandishi wa habari wa Marekani amesema ukandamizaji, dhulma na ukatili unaofanywa na maafisa wa polisi wa Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika umetokana na mafunzo waliyopokea kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kevin Barret amesema aghalabu ya maafisa wa polisi wa Marekani wenye roho za ukatili wamejifunza uovu huo kutoka Israel na kwamba namna wanavyowakandamiza Wamarekani wenye asili ya Afrika, ndivyo Wazayuni wanavyowadhulumu Wapalestina katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu.
Barret amesema licha ya kuwa Washington imekuwa ikijipiga kifua na kudai kuwa Marekani ni nchi huru yenye kuheshimu haki za binadamu, lakini historia inadhihirisha kuwa maafisa usalama wa nchi hiyo wamekuwa wakitumia mkono wa chuma dhidi ya wageni na Wamarekani wenye asili tofauti haswa wenye asili ya Kiafrika.
Jumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu zimekuwa zikikosoa na kulalamikia namna polisi wa Marekani wanavyoamiliana kinyama na Wamarekani weusi.
Mwezi Mei mwaka huu, Rais Barack Obama wa Marekani alikiri kuwa kungali kuna ubaguzi wa rangi na tofauti za kitabaka ndani ya jamii ya nchi hiyo na kutaka zichukuliwe hatua muhimu kukabiliana na suala hilo.