Sisitizo la udharura wa kuweko umoja kati ya Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i18943-sisitizo_la_udharura_wa_kuweko_umoja_kati_ya_waislamu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS amesistiza kuhusu udharura wa kuimarishwa umoja wa Waislamu duniani.
(last modified 2025-11-12T06:10:22+00:00 )
Nov 07, 2016 04:17 UTC
  • Sisitizo la udharura wa kuweko umoja kati ya Waislamu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS amesistiza kuhusu udharura wa kuimarishwa umoja wa Waislamu duniani.

Ayatullah Mohammad Hassan Akhtari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt alisema hayo jana Jumapili alipokutana na maimamu na maulamaa wa jamii ya Waislamu wa nchini Ivory Coast.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wanazuoni hao wa madhehebu za Kishia na Kisunni, Ayatullah Akhtari ameashiria hali ya hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema, suala la umoja ni muhimu sana kati ya Waislamu. Ametoa mwito kwa maulamaa katika jamii za Waislamu kuchukua hatua za kweli za kuelekea kwenye umoja. Aidha ameashiria ujumbe wa umoja wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa, hii ni njia muafaka ya kuvunja njama za maadui wa Uislamu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya  Ahlul Bayt AS amegusia pia sera za nchi za Magharibi za kibeberu na kupora utajiri wa nchi za Afrika na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono wa nchi zinazodhulumiwa na zilizokoloniwa.

Ayatullah Akhtari amewafikishia hadhirina salamu kutoka kwa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema anazingatia kwa kina masuala ya Afrika.

Maulamaa wa madhehebu ya Sunni waliohudhuria mkutano huo wameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa dola kubwa lenye nguvu na ambalo linawaunga mkono Waislamu duniani. Aidha wamesisitiza kuhusu ulazima wa kuwepo umoja miongoni mwa Waislamu duniani.