Iran yazawadia shule za Afrika Kusini vitabu vya masomo ya Kiislamu
Nov 26, 2016 13:09 UTC
Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Afrika Kusini amezizawadia shule za nchi hiyo vitabu kuhusu mafundisho ya Kiislamu.
Taarifa zinasema vitabu hivyo vya mafundisho ya Kiislamu na elimu za kiufundi vimezawadiwa wakuu wa shule mbili mjini Pretoria na Kituo cha Kiislamu cha Johannesburg.
Shule hizo mbili za Pretoria huwa na vikao maalumu kila Jumamosi na Jumapili ambapo wanafunzi hupata anuwai za mafunzo kuhusu Uislamu na Qur'ani Tukufu.
Vitabu hivyo vimetayarishwa kwa lugha ya Kiingereza katika Taasisi ya Utamaduni na Elimu ya Nur Mubin ya Iran kwa utaalamu na kwa kuzingatia umuhimu wa marejeo sahihi na yenye kutumika kwa mujibu wa utamaduni wa Afrika Kusini.
Tags