Dec 21, 2016 14:19 UTC
  • Iran na Armenia zasaini hati tano za ushirikiano

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Armenia zimesaini hati tano za mapatano na makubaliano ya ushirikiano kwa kuhudhuriwa na Marais wa Iran Hassan Rouhani na mwenzake wa Armenia, Serzh Sargsyan.

Hati hizo tano za mapatano ya ushirikiano katika nyanja za utamaduni, utalii, uwekazaji vitega uchumi, michezo na hali za dharura kati ya Iran na Armenia zimesainiwa na maafisa wa nchi mbili hizo. Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo ameelekea mjini Yerevan Armenia kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo. Rais wa Iran alilakiwa rasmi mjini Yerevan na Rais Serzh Sarqsyan wa Armenia. Marais wa Iran na Armenia walikuwa na mazungumzo yaliyotupia jicho kuimarishwa uhusiano kati ya nchi mbili hizo na kuboresha mashirikiano ya pamoja katika nyanja mbalimbali, kieneo na kimataifa, baada ya kupokelewa rasmi ya Rais wa Iran. 

Mazungumzo ya pande mbili kati ya Iran na Armenia mjini Yerevan 

Baada ya kukamilisha safari yake nchini Armenia, Rais Rouhani ataendelea na safari yake ya kiduru katika eneo la Asia ya Kati kwa kuelekea Kazakhstan  na kisha kuhitimishia safari yake hiyo nchini Kyrgyzstan.

Tags