Watu wa Canada wataka bidhaa za Israel zisusiwe
https://parstoday.ir/sw/news/world-i25888-watu_wa_canada_wataka_bidhaa_za_israel_zisusiwe
Watu wa Canada wametaka bidhaa zinazotegenezwa Israel zisusiwe nchini humo kama njia ya kutetea haki za taifa la Palestina.
(last modified 2026-02-02T05:45:46+00:00 )
Mar 03, 2017 13:37 UTC
  • Watu wa Canada wataka bidhaa za Israel zisusiwe

Watu wa Canada wametaka bidhaa zinazotegenezwa Israel zisusiwe nchini humo kama njia ya kutetea haki za taifa la Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika Lisilo la Kiserikali ya "Canada kwa ajili ya Uadilifu na Amani Mashariki ya Kati" uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa, raia wa Canada mbali na kuafiki azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limelaani ujenzi wa vitongozi vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina, pia wametaka utawala wa Israel uwekewe vikwazo .

Aghalabu ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wamelaani vikali namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyokiuka sheria za kimataifa na kwa msingi huo wamesema ni jambo la kimantiki kususia bidhaa za Israel.

Maandamano ya kuunga mkono ususiwaji Israel

Harakati ya kimataifa ya kuiwekea vikwazo Israel inayojulikana kwa jina la Boycott, Divestment and Sanctions against Israel BDS, inaendelea kuimarika kimataifa kutokana na uungaji mkono mkubwa inaopata kutoka kwa jumuiya za viwanda, makundi ya kidini, mashirika yasiyo ya serikali na serikali zinazoungwa mkono na wananchi. Ni wazi kuwa vikwazo ambavyo vimekuwa vikitekelezwa dhidi ya utawala wa Kizayuni vimekuwa na matokeo makubwa hasi ya kisiasa, kidiplomasia, kiutamaduni na kiuchumi kwa utawala huo. Hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel umeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na mafanikio ya harakati hiyo.