Afghanistan yatajwa kuwa nchi ya nne kuathiriwa na vita duniani
Kituo cha kimataifa cha Uchunguzi wa Kistratijia, kimeitaja Afghanistani kuwa nchi ya nne kuathiriwa na vita duniani.
Taarifa iliyotolewa na kituo hicho imesema kuwa, Afghanistan ni nchi ya nne baada ya Mexico, Syria na Iraq ambazo zimeathirika pakubwa na mapigano ya ndani na maafa ya kibinaadamu mwaka 2016.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi za Iraq, Afghanistan, Yemen, Somalia, Sudan, Uturuki, Sudan Kusini na Nigeria ni mataifa yaliyoathirika sana baada ya Mexico na Syria kwa kuwa na maafa makubwa ya kibinaadamu yanayosababishwa na makundi ya wabeba silaha. Kabla ya hapo ofiri ya mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan sambamba na kutoa ripoti iliyoelezea hali mbaya inayotokana na maafa ya kibinaadamu katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzoni mwa mwka huu, ilitangaza kuwa, katika kipindi hicho jumla ya raia 715 waliuawa na wengine zaidi ya 1460 kujeruhiwa.
Kadhalika ripoti hiyo iliongeza kuwa, miji ya Kabul, Helmand, Kandahar, Nangarhar na Urozgan ndio iliyoathirika sana na machafuko nchini humo. Hii ni katika hali ambayo mwaka 2016 jumla ya raia 3000 waliripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 11400 kujeruhiwa idadi ambayo ni mara tatu zaidi ya idadi iliyoripotiwa mwaka 2015.