Jun 05, 2017 06:50 UTC
  • Kiongozi wa upinzani Uingereza aituhumu Saudia kwa kuunga mkono ugaidi

Kiongozi wa upinzani nchini Uingereza, Jeremy Corbyn amesema, wakati sasa umewadia kwa nchi yake kufanya 'mazungumzo magumu' na Saudia Arabia na madola mengine ya Kiarabu ambayo yanaunga mkono magaidi.

Akizungumza baada ya mashambulio ya kigaidi ya mjini London yaliyopelekea jumla ya watu 10 kuuawa wakiwemo magaidi watatu, Jeremy Corbyn kiongozi wa chama cha upinzani cha Leba amesema kuna haja kwa Uingereza kufanya kile alichokitaja kuwa ni mazungumzo magumu na Saudi Arabia na nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi ambazo zinaunga mkono na kuchochea itikadi zenye misimamo mikali.

Corbyn pia amebainisha masikitiko yake kwamba, kumekuwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu baada ya hujuma za hivi karibuni za Uingereza. Ametoa mwito kwa Waingereza kutouchukia Uislamu na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Juni 8 ambapo chama cha Leba kinachuna na chama tawala cha Conservative.

Usalama Waimarishwa London baad aya hujuma ya kigaidi

Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limedai kuhusika na hujuma ya kigaidi ya mjini London ya siku ya Jumamosi.

Hayo yanajiri wakati ambapo hivi karibuni serikali  ya Uingereza ilikosolewa kwa kuficha ripoti inayoihusisha na kuhusika Saudi Arabia katika vitendo vya kigaidi na uungaji mkono wake wa kifedha kwa makundi ya kigaidi yenye misimamo mikali ya Kiwahhabi duniani.

Tags