Aug 27, 2017 14:36 UTC
  • Kansela wa Ujerumani aunga mkono siasa za kuwapokea wakimbizi

Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel ameunga mkono siasa zinazotekelezwa na serikali yake za kuwapokea wakimbizi nchini humo.

Akitangaza msimamo huo leo, Angela Merkel ameunga mkono siasa hizo za serikali yake za kuwakubali wakimbizi na kueleza kuwa hatua hiyo iliyochukuliwa na Berlin ya kuwapokea wakimbizi zaidi ya milioni moja ilikuwa sahihi. 

Kansela wa Ujerumani ameongeza kuwa yeye ametetea hatua yake hiyo ya kuwakaribisha wakimbizi nchini humo licha ya kuwepo hitilafu ndani ya chama tawala cha Christian Democrat Union kuhusu suala hilo. Bi Merkel amebainisha kuwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya zinapaswa kutekeleza majukumu yao katika suala la kuwapokea wakimbizi.

wakimbizi kutoka katika nchi za Mashariki ya Kati wakiwa wamewasili Ulaya 

Itafahamika kuwa akiwa katika kampeni zake za uchaguzi, Angela Merkel amekabiliwa na malalamiko kuhusu siasa zinazotekelezwa na serikali yake kuhusu wakimbizi. Uchaguzi wa bunge la Ujerumani umepangwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu. Merkel ataendelea kushika wadhifa wa Kansela wa Ujerumani kwa mara ya nne iwapo mrengo unaofungamana naye utashinda katika uchaguzi huo wa bunge. 

Tags