EU yazitahadharisha nchi wanachama kutokana na mashambulizi ya kigaidi
Kamishna wa Usalama wa Umoja wa Ulaya, Julian King amezionya nchi wanachama kutokana na wimbi la mashambulizi mapya ya makundi ya kigaidi.
Julian King ameyasema hayo leo ambapo ameonya kwamba baada ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) kushindwa nchini Iraq na Syria, sasa limehamishia uwekezaji wake katika nchi nyingine za kigeni. Ameongeza kuwa, hivi sasa kuna hatari kubwa kwamba baadhi ya pande zitaanzisha uungaji mkono wa kifedha kwa kundi hilo.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limepoteza maeneo yake mengi lililokuwa linayadhibiti nchini Iraq na Syria na sasa linakusudia kuendeleza hujuma zake katika mataifa mengine ikiwemo barani Ulaya. Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa, kundi hilo limeanza kutuma fedha zake nje ya nchi za Iraq na Syria kwa kiwango kidogo na kwamba ni vigumu kuweza kuzitambua fedha za kundi hilo. Ripoti ya Kamishna wa Usalama wa Umoja wa Ulaya imetolewa katika hali ambayo Marekani na madola ya Ulaya ndio waungaji mkono wakuu wa makundi ya kigaidi yenye idolojia ya Uwahabi wa Saudia, katika nchi za Iraq na Syria.
Katika kikao cha nchi wanachama wa kundi la G20 kilochofanyika hivi karivuni mjini Hamburg, Ujerumani, viongozi walioshiriki kikao hicho walishinwa kufikia makubaliano juu ya namna ya kuzuia uungaji mkono wa kifedha kwa makundi ya kigaidi. Suala hilo lilishindikana kutokana na nchi hizo kutokuwa jadi katika kadhia hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa ni madola hayo hayo ndiyo yanayoyafadhili makundi hayo kwa fedha na silaha.