Unicef: Athari hasi za vita zinaathiri ukuaji wa watoto milioni 87
https://parstoday.ir/sw/news/world-i3721-unicef_athari_hasi_za_vita_zinaathiri_ukuaji_wa_watoto_milioni_87
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umeeleza kuwa watoto karibu milioni 87 walio na umri chini ya miaka saba walioko katika maeneo mbalimbali duniani yaliyoathiriwa na vita, wanaishi katika mazingira ambayo yanaaathiri vikali ukuaji wao wa kiakili.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 24, 2016 15:09 UTC
  • Watoto vitani
    Watoto vitani

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umeeleza kuwa watoto karibu milioni 87 walio na umri chini ya miaka saba walioko katika maeneo mbalimbali duniani yaliyoathiriwa na vita, wanaishi katika mazingira ambayo yanaaathiri vikali ukuaji wao wa kiakili.

Shirika la Unicef limetangaza katika taarifa yake kuwa watoto ambao wamaeathirika vibaya kisaikolojia, huwenda wakakabiliwa na ukuaji wao wa kiakili.

Taarifa ya Unicef imeongeza kuwa lishe ya maziwa ya mama, kupata fursa ya kujifunza na ile ya kukulia kwenye mazingira yenye amani na utulivu, ni miongoni mwa mambo chanya yanayosaidia ukuaji wa ubongo wa mtoto katika miaka saba ya mwanzo ya maisha yake.

Unicef imeongeza kuwa watoto mbali na kukabiliwa na vitisho vya kifizikia katika hali za migogoro, hupatwa pia na matatizo ya kinafsi.