Jun 25, 2018 07:32 UTC
  • Rais Erdoğan wa Uturuki atangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa jana

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini Uturuki (YSK) amemtangaza rasmi Rais Recep Tayyip Erdoğan kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili ya jana nchini humo.

Saadi Gwon amesema kuwa, Rais Erdoğan ameshinda uchaguzi huo. Kwa mujibu wa Gwon, Erdoğan ameshinda kwa asilimia 97.7 ya kura. Aidha ameongeza kwamba, matokeo rasmi ya uchaguzio huo wa rais na bunge yatatangazwa ndani ya siku tano zijazo. Hii ni katika hali ambayo asubuhi ya leo Rais Recep Tayyip Erdoğan alijitangazia kwamba yeye ndiye aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo. Katika taarifa aliyoitoa kwa taifa, Erdoğan alisema kuwa kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi, ameibuka mshindi katika uchaguzi huo. Aidha aliwashukuru Waturuki kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na kuutaja kuwa ushindi wa kidemokrasia. Kadhalika alikitaja kiwango cha ushiriki wa uchaguzi wa jana kuwa ni asilimia 90. Duru ya 26 ya uchaguzi wa bunge na pia uchaguzi wa kwanza wa rais katika mfumo wa urais nchini Uturuki, ilifanyika Jumapili ya jana Juni 24.

Kampeni za uchaguzi uliopita

Licha ya ushindi wa Rais Recep Tayyip Erdoğan, chama kikuu cha upinzani nchini humo, kimesisitiza kwamba ni mapema sana kukubali kushindwa. Katika uchaguzi huo wa rais wagombea sita walichuana vikali. Hivi karibuni Erdoğan alisema kuwa Wamagharibi wanasubiri kushindwa kwake katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo na kwamba raia wa Uturuki wamejiandaa kutoa somo kwa nchi hizo. 

Tags