Jun 30, 2018 07:51 UTC
  • Human Rights Watch yakosoa sera za Donald Trump

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekosoa vikali sera za hivi karibuni za serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani.

Mtandao wa Human Rights Watch mbali na kukosoa mipango na sera za hivi karibuni za serikali ya Trump umesisitiza kuwa, katika uwanja wa sera zake za ndani na  za nje, serikali ya Marekani imepuuza suala la haki za binadamu.

Ukosoaji huo wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch umekuja baada ya Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na Nikki Haley balozi na mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa kutangaza habari ya kujitoa nchi yao katika Baraza la Haki za Binadamu la UN hatua ambayo ni uungaji mkono kwa utawala haramu wa Israel.

Rais Donald Trump wa Marekani

Katika upande mwingine, Zeid Ra'ad al Hussein Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amekuwa akikosoa vikali hatua ya serikali ya Marekani ya kuwatenganisha kwa nguvu watoto na wazazi wao wahajiri  na kueleza kwamba, hatua hiyyo haifai na inapaswa kulaaniwa.

Marekani ambayo imekuwa ikidai kuwa mtetezi wa haki za binadamu na hata kuzishinikkiza na kuziwekea vikwazo nchi nyingine kwa madai ya kkukiuka haki za binadamu, yenyewe imekuwa kinara wa kukkiuka haki za binadamu na kuuunga mkono tawala zinazotenda jinai kama Israel na Saudi Arabia.

Tags