Askari wa UN akiri kunajisi watoto wadogo Afrika
Askari mmoja wa zamani wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekiri kwamba, aliwanajisi watoto na wanawake wa Kiafrika wakati alipokuwa akihudumia kikosi hicho mwaka 2004.
Gazeti la Sanday Times la Uingereza limeripoti kuwa, Didier Bourguet ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha huduma za magari ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Goma huko mashariki kwa Congo DR amekiri kwamba, hakumbuki ni watoto wangapi aliowanajisi alipokuwa katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.
Gazeti la Sunday Time limeripoti kuwa Didier Bourguet ambaye ni raia wa Ufaransa ni sehemu ya utamaduni unaotawala baina ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambao wamepatwa na maradhi ya ufuska wa kingono katika nchi wanakohudumu.

Mwaka 2008 mahakama moja ya Ufaransa ilimhukumu Didier Bourguet kifungo cha miaka 9 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi zaidi ya watoto 20 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Gazeti la Sunday Times limeongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni wanajeshi na wahudumu wasio wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa wanaujulikana kwa jila la kikosi cha Kofia Blue wamekabiliwa na tuhuma za kubaka na kunajisi watoto na wanawake katika nchi mbalimbali hususan barani Afrika.