Bangladesh: Myanmar imetutaka tuache kuwasaidia wakimbizi wa Rohingya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47411-bangladesh_myanmar_imetutaka_tuache_kuwasaidia_wakimbizi_wa_rohingya
Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh imesema kuwa, Myanmar imeitaka serikali ya nchi hiyo kusimamisha misaada ya kibinaadamu kwa malaki ya wakimbizi wa Rohingya walioko katika maeneo ya mpaka wa nchi mbili.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 13, 2018 07:38 UTC
  • Bangladesh: Myanmar imetutaka tuache kuwasaidia wakimbizi wa Rohingya

Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh imesema kuwa, Myanmar imeitaka serikali ya nchi hiyo kusimamisha misaada ya kibinaadamu kwa malaki ya wakimbizi wa Rohingya walioko katika maeneo ya mpaka wa nchi mbili.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema kuwa, katika mazungumzo yaliyofanyika kati ya viongozi wa Myanmar na Bangladesh mjini Naypyidaw, mji mkuu wa Myanmar, kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa nchi hiyo aliitaka serika serikali ya Dhaka kusitisha misaada hiyo ya kibinaadamu kwa wakimbizi hao Waislamu. Wakati huo huo wakimbizi hao sambamba na kuonyesha wasi wasi wao mkubwa kutokana na hali yao mbaya wamesema kuwa, mashinikizo ya hivi karibuni ya viongozi wa serikali ya Myanmar dhidi yao, yameifanya hali ya mambo kuwa mbaya zaidi.

Abul Hassan Mahmood Ali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bangladesh

Kabla ya hapo Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa jeshi la Myanmar limehusika wa mauaji ya kibaguzi nchini humo sambamba na kulitaja jeshi hilo kuwa jeshi baya zaidi duniani. Aidha Shirika la Msalaba Mwekundu limetangaza kwamba, hali ya sasa nchini Myanmar haifai kwa ajili ya kuwarejesha wakimbizi Waislamu wa Rohingya. Tangu tarehe 25 mwaka jana, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha magaidi lilianzisha mashambulizi makali dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine, magharibi mwa nchi hiyo ambapo zaidi ya Waislamu elfu sita waliuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa. Aidha katika jinai hizo wanawake na mabinti wa Kiislamu walibakwa huku makazi yao yakiteketezwa kwa moto na askari hao.