Rais Donald Trump wa Marekani: Kamwe sitomsamehe Barack Obama
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49414-rais_donald_trump_wa_marekani_kamwe_sitomsamehe_barack_obama
Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kumkosoa vikali mtangulizi wake, Barack Obama amesema: 'Kamwe sitomsamehe Obama kutokana na hatua yake ya kulidhoofisha jeshi na masuala mengine mengi.'
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 10, 2018 04:47 UTC
  • Rais Donald Trump wa Marekani: Kamwe sitomsamehe Barack Obama

Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kumkosoa vikali mtangulizi wake, Barack Obama amesema: 'Kamwe sitomsamehe Obama kutokana na hatua yake ya kulidhoofisha jeshi na masuala mengine mengi.'

Trump aliyasema hayo Ijumaa ya jana kabla ya kuanza safari kuelekea nchini Ufaransa ambapo akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusiana na matamshi ya hivi karibuni ya Michelle Obama, mke wa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amesema kuwa, kamwe hatomsamehe mtangulizi wake huyo. Katika kitabu cha kumbukumbu zake ambacho anatazamiwa kukisambaza hivi karibuni, Michelle Obama amemkosoa vikali Trump na kusema kuwa, kutokana na kula njama dhidi ya mume wake, rais huyo wa sasa wa Marekani alitilia shaka uraia wa Obama msimamo ambao ulisukumwa na chuki na hivyo kuhatarisha usalama wa familia ya rais huyo wa zamani wa Marekani.

Mgogoro kati ya Trump na Barack Obama

Kwa mujibu wa Michelle Obama, kamwe hatomsamehe Trump kutokana na kitendo chake hicho. Katika radiamali yake Trump amesema kuwa, hatomsamehe Obama kwa kile alichodai kuwa ni kulidhoofisha jeshi la Marekani. Kwa mujibu wa Rais Donald Trump, katika kipindi cha Barack Obama, jeshi la nchi hiyo liliporomoka, kuzeeka na kuchoka na kwamba baada ya yeye kuingia madarakani ndipo likapata nguvu. Mgogoro kati ya Trump na Obama ulishtadi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mdogo uliopita nchini humo ambapo kwa mara kadhaa pande mbili zilikuwa zikishambuliana kuhusu masuala ya ndani na nje ya Marekani.