Dec 04, 2018 07:34 UTC
  • Kwa mara nyingine Trump aiomba Kongresi imruhusu kujenga ukuta mpakani

Rais wa Marekani amesema kuwa nchi hiyo itatumia mabilioni ya dola kwa ajili ya kujenga ukuta katika mipaka ya nchi hiyo na Mexico iwapo Wademocrat katika kongresi ya nchi hiyo wataafiki bajeti ya ujenzi huo.

Rais wa Marekani, Donald Trump jana Jumatatu alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akikariri msimamo wake wa kibaguzi wa kupinga wahajiri ambapo aliandika kuwa: Kivyovyote vile wahajiri hawataruhusiwa kuvuka mipaka na kuingia Marekani kinyume cha sheria; na iwapo italazimika Marekani itafunga mipaka yake yote ya kusini. 

Rais mbaguzi wa Marekani Donald Trump 

Rais huyo wa Marekani Jumatano iliyopita pia alitishia kuwa serikali yake itasitisha shughuli zake iwapo kongresi ya nchi hiyo  haitatoa kibali cha kutolewa bajeti ya lazima ya dola bilioni tano kwa ajili ya kujenga ukuta katika mpaka ya nchi hiyo na Mexico. Trump ameitishia pia kongresi ya Marekani kwamba huwenda akatafuta mbinu nyingine za kutekeleza mpango huo ili kutimiza lengo alilokusudia yaani kujenga ukuta huo baina ya mpaka ya Marekani na Mexico iwapo haitapasisha bajeti ya lazima ya ufanikishaji wa zoezi hilo. Aidha alisema ataamuru kutumwa wanajeshi wa Marekani katika maeneo hayo ya mpakani na kuweka uzio wa senyenge na chuma ili kuzuia kuvuka wahajiri wa Kimexico kuelekea nchini Marekani. 

Tags