Nov 27, 2019 08:11 UTC
  • Raia weusi 3 wa Marekani waachiwa huru baada ya kufungwa jela bila ya hatia kwa miaka 36

Wamarekani 3 weusi wameachiwa huru baada ya kufungwa jela kwa kipindi cha miaka 36 kwa tuhuma za kufanya mauaji.

Ripoti zinasema kuwa, Wamarekani hao watatu wenye asili ya Afrika walikuwa barobaro wakati walipohukumiwa kifungo mwaka 1983 kwa tuhuma za kumuua mtoto aliyekuwa na umri wa miaka 14 lakini sasa baada ya kifungo cha miaka 36 wendesha mashtaka wa Marekani wamekiri kwamba, walifanya makosa kuwahuku kifungo na kutangza kuwa Wamarekani hao hawakuwa na makosa na kwamba mtoto huyo aliuawa na mtu mwingine.

Wamarekani hao sasa wana umri wa miaka 50 na wamemaliza miaka 36 ya umri wao wakiwa jela bila ya kufanya kosa lolote.

Baada ya kuachiwa huru Wamarekani hao waliotambulika kwa majina ya Alfred Chestnut, Andrew Stewart and Ransom Watkins wamewaambia waandishi wa habari kuwa, miaka yote waliyokuwa jela wamekuwa wakisisitiza kwamba hawajafanya kosa lolote lakini vyombo vya sheria vya Marekani vilipuuza maneno yao. 

Mwaka jana wa 2018 pia mahakama ya Marekani katika jimbo la Kansas ilimwachia huru Mmarekani mwingine mwenye asili ya Afrika aliyejulikana kwa jina la Lamonte McIntyre baada ya kufungwa jela miaka 23 bila hatia yoyote kwa tuhuma ya kuhusika na mauaji ya watu wawili. 

Ubaguzi dhidi ya Wamarekani weusi umeongezeka

Wanaharakati wa masuala ya kiraia wanatahadharisha kwamba, ubaguzi dhidi ya jamii ya Wamarekani weusi unazidi kuongeza nchini humo katika miaka ya hivi karibuni hususan baada ya Rais Donald Trump kushika madaraka ya nchi. 

Tags