Dec 02, 2019 04:43 UTC
  • Watu 54 wauawa au kujeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi Marekani

Idara ya Takwimu za Utumiaji Silaha kwa Mabavu Marekani imesema watu 54 wameuawa au kujeruhiwa katika vitendo vya ufatulianaji risasi nchini humo katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Kwa mujibu wa Taarifa ya idara hiyo iliyochapishwa Jumapili, katika matukio 55 ya ufaytulianaji risasi Marekani katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita katika majimbo mbali mbali ya nchi hiyo, watu wasiopungua 21 wameuawa papo hapo na wengine 33 kujeruhiwa.

Vitendo hivyo vya ukatili vimeripotiwa katika majimbo ya Louisiana, Texas, Florida, na Washington DC. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kipindi cha masaa 48 yliyopita, kumekuwa na vitendo  156 vya ufyatulianaji risasi katika majimbo mbali mbali ya Marekani ambapo watu 52 wameuawa na wengine 108 wamejeruhiwa.

Kila mwaka maelfu ya Wamarekani hupoteza maisha kwa kufyatuliwa risasi katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

Rais Trump wa Marekani ni muungaji mkono mkubwa wa wafanya biashara wa silaha ambazo zinaangamiza maelfu ya Wamarekani kila mwaka

Pamoja na kuwa watetezi wa haki za raia wametaka kuwepo sheria kali za umiliki wa silaha, lakini mashirika makubwa ya utengenezaji na uuzaji silaha ya Marekani yametumia ushawishi wao kuzuia sheria hiyo kutekelezwa. Rais Donald Trump ni mmoja kati ya waungaji mkono wakubwa wa mashirika hayo yanayojihusisha na biashara ya silaha nchini Marekani.

Mwanzoni mwa urais wake, Trump alitangaza bayana kuwa, miaka minane ya kukiukwa haki za wenye silaha imefika ukingoni kwani wana muungaji mkono mkubwa katika Ikulu ya White House.

Tags