Moscow yatahadharisha kuhusu vikwazo vya Marekani dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Chechniya
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametahadharisha kuwa Moscow itatoa jibu kwa vitisho vya Washington dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Chechniya inayojiendeshea mambo yake yenyewe.
Hatua ya Marekani ya kutangaza kumuwekea vikwazo Rais Ramzan Kadyrov wa Jamhuri ya Chechniya inayojiendeshea mambo yake yenyewe, mkewe na mabinti wake wawili kwa tuhuma za kukiuka haki za binadamu imekabiliwa na radiamali ya Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia.

Maria Zakharova amepinga hatua ya karibuni ya Marekani dhidi ya Russia ya kumuwekea vikwazo Rais wa Jamhuri ya Chechniya inayojiendeshea mambo yake yenyewe na familia yake; na kusisitiza kuwa Moscow itajibu hatua hiyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema na hapa ninamnukuu, "kulipiza kisasi si hatua rahisi lakini tutapata njia ya kujibu hatua hiyo."
Kwa mujibu wa Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, vikwazo hivyo vinawajumuisha mke wa rais wa Jamhuri ya Chechniya na mabinti zake wawili.