Wendy Sherman: Iran imechagua stratejia ya muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62646-wendy_sherman_iran_imechagua_stratejia_ya_muqawama
Afisa wa zamani wa Marekani amezitaja siasa za White House dhidi ya Iran kuwa zisizo na natijana na kusisitiza kuwa Iran imechagua stratejia ya muqawama.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 06, 2020 08:07 UTC
  • Wendy Sherman: Iran imechagua stratejia ya muqawama

Afisa wa zamani wa Marekani amezitaja siasa za White House dhidi ya Iran kuwa zisizo na natijana na kusisitiza kuwa Iran imechagua stratejia ya muqawama.

Bi Wendy Sherman aliyekuwa Naibu Waziri wa Mashauri wa Kigeni wa Marekani katika serikali ya Rais Barak Obama amesema kuwa Iran kivyovyote vile haiko karibu na mazungumzo. Sherman ameyasema hayo jana katika Mkutano wa Usalama cha Aspen uliofanyika kwa njia ya video.  Afisa huyo wa zamani wa Marekani amesisitiza kuwa, kwa msingi huo "tupo katika nukta mbaya sana." 

Wendy Sherman wakati huo huo amejibu madai ya Briah Hook Mjumbe Maalumu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani Katika Masuala ya Iran kwa kusema: "Vivi sasa hatuna mapatano baada ya kufikiwa mapatano ya nyuklia mwaka 2015, na Iran imerutubisha asilimia zaidi za uranium." 

Brian Hook amekariri tena madai yake yasiyo na msingi kuhusu Iran katika Mkutano wa Usalama wa Aspin na kusema kuwa Tehran inapasa kuchagua moja ima mashinikizo ya kiuchumi au mazungumzo. 

Brian Hook, Mjumbe Maalumu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani Katika Masuala ya Iran

Katika mkutano huo naye Mark Esper Waziri wa Ulinzi wa Marekani amekariri misimamo ya viongozi wa serikali ya Trump dhidi ya Iran na kusema: Siasa za Pentagon ni kwa ajili ya kuimarisha waitifaki wa kieneo wa Washington kama Israel na Saudi Arabia ili kukabiliana na Iran. 

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, marufuku za silaha ilizowekewa Iran zitaondolewa tarehe 18 mwezi Oktoba mwaka huu kwa mujibu wa vipengee vya azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa licha ya hatua na matamshi yote hayo ya viongozi wa White House dhidi ya Iran. 

Russia na China ambazo ni miongoni mwa nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama hadi sasa zimepinga mara kadhaa kurefushwa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.