Oct 09, 2020 07:48 UTC
  • Msafara wa

Msafara kwa jina la Ujumbe wa Arubaini umewasili katika mji wa Milan nchini Italia ukiwa katika safari yake barani Ulaya.

Kundi linalowakutanisha pamoja wapenzi na maashiki wa Ahlu Bait wa Mtume Mtukufu wa Uislamu (S.A.W) barani Ulaya lililianza safari yake hiyo ya kimataifa kwa lengo la kuwafahamisha raia wa Ulaya kuhusu marasimu ya Arubaini na utamaduni wa Hussein (as). Jana alasiri kundi hilo la wapenzi wa Ahlul Bait wa Mtume liliwafikishia ujumbe wa Arubaini wananchi wa Italia katika maidani kubwa zaidi na muhimu sana katika mji wa Milan kwa kugawa maji, maua na kuwasiliana nao kikamilifu.

Msafara huo ulianza safari yake katika nchi 10 za Ulaya  Ijumaa iliyopita katika maidani ya Uholanzi na hadi sasa tayari imeshapita katika nchi za ubelgiji, Ufaransa na Uswisi na sasa umefika Italia. 

Kituo kinachofuata cha msafara huu wa Ujumbe wa Arubain kitakuwa ni Slovenia. Wapenzi wa Imam Hussein (a.s) mwaka huu wameshindwa kushiriki katika matembezi ya Arubaini kutokana na janga la Corona; na imeamuliwa kwamba familia zisome ziyara ya Arubaini majumbani kwa kufuata miongozo ya afya. 

Marasimu ya Arubaini katika mji wa Karbala  kabla ya janga la corona 

 

Tags