Asilimia 80 ya Wamarekani wanaamini Trump amepigwa na chini, vurugu zinaendelea
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64570-asilimia_80_ya_wamarekani_wanaamini_trump_amepigwa_na_chini_vurugu_zinaendelea
Huku hali ya vurugu na wasiwasi ikizidi kuiandamana Marekani na kufanya asilimia yao kubwa kutokuwa na imani na madai ya demokrasia nchini humo, uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni nchini humo unaonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi hao wanaamini kwamba Donald Trump anang'ang'ania madaraka bila sababu kwani ameshindwa katika uchaguzi wa Novemba 3, 2020.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 12, 2020 02:47 UTC
  • Asilimia 80 ya Wamarekani wanaamini Trump amepigwa na chini, vurugu zinaendelea

Huku hali ya vurugu na wasiwasi ikizidi kuiandamana Marekani na kufanya asilimia yao kubwa kutokuwa na imani na madai ya demokrasia nchini humo, uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni nchini humo unaonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi hao wanaamini kwamba Donald Trump anang'ang'ania madaraka bila sababu kwani ameshindwa katika uchaguzi wa Novemba 3, 2020.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na shirika la habari la Reuters na Taasisi ya Ipsos yanaonesha kuwa, karibu asilimia 80 ya Wamarekani wakiwemo zaidi ya nusu ya wafuasi cha chama cha Trump cha Republican wanaamini kwamba Joe Viden ndiye aliyeshinda katika uchaguzi huo. Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi huo mpya wa maoni, asilimia 79 ya watu wazima nchini Marekani wanaamini kwamba Joe Biden ameshinda katika uchaguzi wa Novemba 3. Vile vile matokeo ya uchunguzi huo yanaonesha kuwa, karibu asilimia 60 ya wanachama wa chama cha Republican cha Donald Trump pamoja na wananchi wote wa chama cha Democratic wanaamini kwamba Biden ndiye mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne, Novemba 3, 2020.

Trump na Biden

 

Huku hayo yakiripotiwa, televisheni ya Fox News imetangaza kuwa, kutokana na namna uchaguzi wa rais wa Marekani ulivyoendeshwa, wananchi wa nchi hiyo hawana imani tena na demokrasia. Fox New imeeleza katika ripoti kwamba, raia wa Marekani sasa hawana tena imani na demokrasia. Kanali hiyo ya televisheni imeashiria mchakato wa uchaguzi wa rais wa Marekani ulivyokuwa na kueleza kwamba, makumi ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo wanaitakidi kwamba kura zao katika uchaguzi huo zimeibwa. Ripoti ya Fox News imesema "tunaishi katika nchi ambayo watu hawana imani tena na demokrasia". Kwa mtazamo wa televisheni hiyo, hatua zilizochukuliwa baada ya uchaguzi nchini Marekani zinaandaa mazingira ya kuifanya hali ya mambo iwe mbaya zaidi na kwamba "hali iliyopo sasa ni ya hatari na inaweza ikawa ya hatari zaidi."