Nov 15, 2020 08:09 UTC
  • Wafuasi na wapinzani wa Trump wapigana Washington, Marekani

Maandamano ya wafuasi wa rais wa Marekani, Donald Trump mjini Washington DC yameingia kwenye machafuko baada ya kuzuka mapigano baina yao na watu wanaopinga ubaguzi wa rangi.

Televisheni ya Russia Today imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wafuasi wa Donald Trump wamefanya maandamano wakidai kuibiwa kura na walielekea kwenye jengo la Mahakama Kuu ya mji huo. Wafuasi wa magenge ya mirengo ya kulia yenye misimamo mikali ambao mengi wao walikuwa na silaha, wameshiriki kwenye maandamano hayo. Waandamanaji hao wamepigana na kundi moja la Wamarekani wneye asili ya Afrika ambao nao walikuwa wamekusanyika kumpinga Donald Trump. Jeshi la polisi lililazimika kuingilia kati kuzima mapigano hayo. Rais huyo wa Marekani alijitokeza mbele ya wafuasi wake katika maandamano hayo ili kuonesha anaunga mkono ubaguzi wa rangi wa magenge hayo ambayo yanaamini kwamba wazungu ni bora kuliko watu wa jamii nyingine.

Donald Trump aliyebwagwa nchini Marekani

 

Donald Trump alishiriki maandamano hayo kuunga mkono pote la wabaguzi hao wa rangi na kusahau kwamba yeye ni rais wa nchi yenye watu wa rangi na vizazi tofauti. Mara kadhaa alirudia kusema kwamba mfumo wa uchaguzi wa Marekani ni mbovu na mharibifu kupindukia. Msemaji wa White House, Kayleigh McEnany, amedai kuwa zaidi ya wafuasi milioni moja wa Trump wameshiriki kwenye maandamano hayo. Hata hivyo picha za vyombo vya habari zinaonesha kulikuwa na elfu kadhaa tu ya wafuasi wa Trump katika maandamano hayo. Licha ya takwimu za vyombo vya habari vya Marekani kuonesha kuwa, Donald Trump amebwagwa vibaya katika uchaguzi wa rais wa Novemba 3, 2020, lakini bado rais huyo anang'ang'ania kuwa yeye ndiye mshindi. Amefungua mashtaka mahakamani kulalamikia uchaguzi huo. 

Tags