Mwanasayansi wa Marekani atahadharisha, asema kutaibuka COVID-26 na COVID-32
https://parstoday.ir/sw/news/world-i70796-mwanasayansi_wa_marekani_atahadharisha_asema_kutaibuka_covid_26_na_covid_32
Mwanasayansi wa Marekani ameonya kwamba, kutajitokeza COVID-26 na COVID-32 iwapo hatufanyika uchunguzi wa kina wa kubaini asili na chanzo cha virusi vya Corona vinavyosababisha maradhi ya COVID-19.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2021 21:59 UTC
  • Mwanasayansi wa Marekani atahadharisha, asema kutaibuka COVID-26 na COVID-32

Mwanasayansi wa Marekani ameonya kwamba, kutajitokeza COVID-26 na COVID-32 iwapo hatufanyika uchunguzi wa kina wa kubaini asili na chanzo cha virusi vya Corona vinavyosababisha maradhi ya COVID-19.

Peter J. Hotz, mkuu wa kitengo cha tiba katika Chuo cha Baylor huko Marekani, amesema kutaibuka COVID-26 na COVID-32 iwapo hatutajua asili ya COVID-19.

Daktari Hotz amesisitiza kwamba, uchunguzi wa wa kujua asili na chimbuko la COVID-19 unaweza kuzuia magonjwa ya milipuko ya baadaye.

Wataalamu wa nchi za Magharibi wanasema kuna haja kubwa ya kuchunguza asili na chanzo cha vuirusi vya corona na wanaitaka China kuruhusu uchunguzi mpana zaidi kuhusiana na kirusi hicho.

Siku ya Jumatano iliyopita, Rais wa Marekani, Joe Biden aliyaagiza mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo kuzidisha bidii ya kupata chanzo na asili ya virusi vya corona na ameyapa siku 90 kuchunguza nadharia mbili zinazosema kwamba, virusi hivyo vilitoka kwa bahati mbaya kwenye maabara nchini China, au kwamba vilisambaa kwanza kutoka kwa mnyama kwenda kwa wanadamu nje ya maabara.

Wasiwasi wa wanasayansi unaelekezwa zaidi kwenye Taasisi ya Virolojia ya Wuhan nchini China ambayo kwa muda mrefu ilikusanya virusi vya popo na kufanya majaribio katika maabara yake.

Hata hivyo chunguzi uliofanywa mwaka huu na Shirika la Afya Duniani (WHO) ulikanusha uwezekano wa virusi hivyo kutoka kwenye taasisi hiyo.

Wanasayansi wanataka kujua asili ya virusi vya corona

Itakumbukwa kuwa virusi vya corona viliibuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan wa mkoa wa Hubei nchini China na baadaye vikaenea katika nchi nyingine za dunia.

Hadi sasa virusi hivyo vimeua zaidi ya watu milioni tatu na nusu katika maeneo mbalimbali ya dunia.