Russia: Wanajeshi wa Marekani nchini Syria ni wavamizi, waondoke
https://parstoday.ir/sw/news/world-i71072-russia_wanajeshi_wa_marekani_nchini_syria_ni_wavamizi_waondoke
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wanajeshi wa Marekani ni wavamizi nchini Syria na wako huko kinyume cha sheria, hivyo wanapaswa waondoke.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2021 07:08 UTC
  • Russia: Wanajeshi wa Marekani nchini Syria ni wavamizi, waondoke

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wanajeshi wa Marekani ni wavamizi nchini Syria na wako huko kinyume cha sheria, hivyo wanapaswa waondoke.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Sergey Lavrov amesema hayo katika hotuba maalumu na kuongeza kuwa, hakuna sheria yoyote inayohalalisha kuweko wanajeshi wa Marekani nchini Syria.

Hadi hivi sasa Marekani imezuia kinyume cha sheria, mamilioni ya dola ya mali za Syria na mara kwa mara inaiwekea vikwazo nchi hiyo ya Kiarabu ili kutangaza uungaji mkono wa wazi wa Washington kwa magenge ya kigaidi yanayofanya jinai dhidi ya wananchi na maafisa wa serikali ya Syria.

Sergey Lavrov

 

Nchi ya Kiarabu ya Syria iitumbukizwa kwenye mgogoro mwaka 2011 baada ya madola ya kibeberu na vibaraka wao kumimina mamia ya maelfu ya magaidi ndani ya ardhi ya Syria kutoka kila kona ya dunia. Mabeberu hao kwa kushirikiana na vibaraka wao kama Saudi Arabia walimimina magaidi hao nchini Syria kwa kutumia kila kona ya nchi hiyo na fedha nyingi. Madola ya kibeberu yaliyokuwa mstari wa mbele katika jinai hiyo ni Marekani, Ufaransa na Uingereza. Lengo lao lilikuwa ni kulidhoofisha taifa la Syria ambalo ni nguzo muhimu sana katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye eneo hili.

Hata hivyo jeshi la Syria kwa msaada wa washauri wa kijeshi wa Iran na msaada wa Russia limefanikiwa kusambaratisha njama hizo na kulingamiza genge la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini humo.