Visingizio vinavyotumiwa na Marekani kuzuia misaada kwa nchi maskini duniani
-
Janet Yellen
Wakati maambukizi ya virusi vya corona na ugonjwa wa COVID-19 vikiendelea kusababisha mgogoro wa kiuchumi na umaskini katika nchi mbalimbali duniani na kuzifanya nchi hizo zihitajie misaada zaidi ya nchi tajiri, maafisa wa serikali ya Marekani wanafanya mikakati ya kuzuia misaada kwa nchi hizo kwa kutumia visingizio vya aina mbalimbali.
Katika uwanja huo Waziri wa Biashara wa Marekani, Janet Yellen amedai kuwa, nchi maskini zinatumia misaada ya kifedha ya kimataifa kwa ajili ya kulipia madeni yao kwa China.
Wimbi la maambukizi ya virusi vya corona na sheria kali za kuzuia au kupunguza maambukizi ya virusi hivyo ambazo ziliambatana na kusitishwa kazi na shughuli mbalimbali za uzalishaji katia nchi nyingi vimezidisha matatizo ya kiuchumi katika nchi hizo hususan nchi maskini. Kwa kadiri kwamba, zinahitaji misaada na mikopo ya taasisi za kimataifa na nchi tajiri kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao katika kipindi hiki kigumu. Katika upande mwingine nchi nyingi maskini zinakabiliwa na maatizo katika kulipa madeni yao.
Ripoti za mashirika ya kimataifa ziaonesha kuwa, zaidi ya nchi 73 duniani zinalazimika kulipa madeni yao yanayokadiriwa kuwa karibu dola bilioni 33 na milioni 700 hadi kufikia mwishon mwa mwaka huu wa 2021. Hii ni pamoja na kuwa, jumuiya za kimataifa kama shirika la Amnesty International zimezitaka nchi tajiri zifute madeni ya nchi maskini sana hadi kufikia kwa uchache miaka miwili ijayo. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva amesema mambukizi ya virusi vya corona duniani yamezidisha umaskini na ukosefu wa usawa na ametahadharisha kuwa: Mwaka huu uchumi wa dunia unakabilwia na mdororo mkubwa.. Inatupasa kuungana kwa ajili ya kuzisaida nchi maskini sana na chumi zilizopatwa na madhara makubwa hususan nchi ambazo zinazosumbuliwa na madeni makubwa."

Licha ya maagizo na miito yote inayotolewa na taasisi za kimataifa lakini hadi sasa misaada inatolewa kwa nadra sana kwa nchi maskini. Marekani ambayo ni miongoni waw nchi zinazoweza kuzisaidia nchi nyingi maskini hasa za Afrika zinazozongwa na matatizo ya kiuchumi, imesimamisha au kupunguza sana misaada hiyo kwa kutumia visingizio mbalimbali. Maafisa wa serikali ya Washington wameitumbukiza hata China katika suala hilo kama kisingizio cha kinachotumiwa na Washington kukwepa majukumu yake ya kimataifa kwa kudai kuwa, misaada inayotolewa kwa nchi maskini inatumika kulipa madeni ya nchi hizo kwa China.
Hii ni licha ya kwamba, kundi linaloundwa na nchi zenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani ambazo zinadhibiti asilimia 85 ya uchumi wa dunia, zimetangaza kuwa, zimefanya mazungumzo na China na kufanikiwa kuishawishi ishiriki katika mazungumzo yatakayojadili suala la kuchelewesha muda wa kulipwa madeni ya nchi maskini za Kiafrika kwa nchi hiyo.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema thuluthi moja ya chumi zinazoinukia zinakabiliwa na hatari ya mgogoro wa bajeti na ametahadharisha kuwa: Tunakaribia kutumbukia kwenye mgogoro wa madeni.

Kwa kutilia maana mgogoro wa sasa wa virusi vya corona duniani, kuna ulazima wa nchi tajiri kulipa uzito mkubwa zaidi suala la kuzisaidia nchi maskini na kutupilia mbali sera za ubaguzi katika ugavi wa dawa na chanjo ya COVID-19. Hivyo basi, visingizio na bwabwaja za kisiasa kama zile zilizotolewa na Waziri wa Biashara wa Marekani kuhusiana na China haziwezi kukubaliwa na walimwengu.