Mtaalamu wa jeni: Kuna uwezekano COVID-19 haikuanzia Wuhan, China
https://parstoday.ir/sw/news/world-i74652-mtaalamu_wa_jeni_kuna_uwezekano_covid_19_haikuanzia_wuhan_china
Mtaalamu wa jeni amesema, kuna uwezekano kwamba ugonjwa wa COVID-19 haukuanzia katika mji wa Wuhan huko China.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 14, 2021 10:33 UTC
  • Mtaalamu wa jeni: Kuna uwezekano COVID-19 haikuanzia Wuhan, China

Mtaalamu wa jeni amesema, kuna uwezekano kwamba ugonjwa wa COVID-19 haukuanzia katika mji wa Wuhan huko China.

Peter Forster ambaye ni mtaalamu wa jeni na Makamu Mkuu wa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Cambridge ya Masuala ya Utafiti ameeleza kuwa, dhana kwamba ugonjwa wa COVID-19 ulianzia katika soko la vyakula vinavyovunwa kutoka baharini huko Wuhan ni ya upotoshaji.

Hadi sasa watu milioni 219 wamepatwa na maambukizi ya kirusi cha corona duniani na zaidi ya milioni 4.5 wameuawa na virusi hivyo. 

Mtaaalamu huyo wa jeni kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge ameongeza kuwa, aina za spishi za kirusi cha corona zilizosababisha maambukizi makubwa duniani zikiwemo spishi za Delta na Beta zinaweza kujulikana chanzo chake kulingana na mabadliko yaliyotokea nchini Italia.

Timu ya Forster ilichunguza hifadhi data ya asili ya taarifa za kijenetiki kuhusu virusi zilizochukuliwa katika awamu ya kwanza ya wagonjwa wa COVID-19 kati ya Disemba 2019 na mwezi Machi mwaka 2020. Baadaye timu hiyo ilifanikiwa kugundua kirusi chenye umri mkubwa walichokipa jina la Type A. Timu hiyo ilifikia natija kuwa, kirusi hicho hakikuwa kile kilichogunduliwa awali huko Wuhan na kwamba kilianzia sehemu nyingine na kubadilika kabla ya kuwasili katika mji wa Wuhan. 

Soko la vyakula vya baharini la Wuhan, China