-
Uungaji Mkono wa Ulaya kwa Jinai za Israel Umekuwa na Matokeo Gani?
May 04, 2026 12:37Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ametoa indhari kali akisema, nchi za Ulaya zinazizoesha jamii zao sera za kikatili za Israel, yakiwa ni matokeo ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kijeshi na kibiashara na utawala huo wa kizayuni licha ya kuwa unakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika mahakama za kimataifa.
-
John Mearsheimer: Vita dhidi ya Iran ni kushindwa mutlaki Marekani
May 04, 2026 10:27Mnadharia wa mahusiano ya kimataifa wa Marekani, John Mearsheimer, amevitaja vita dhidi ya Iran kuwa ni kosa lenye janga kubwa zaidi katika historia ya sera za kigeni na kushindwa kabisa kwa Marekani.
-
Mwandishi wa habari wa Marekani amwita Trump "mateka wa Netanyahu"
May 04, 2026 10:16Mchambuzi wa Marekani, Tucker Carlson amemtaja Donald Trump kama mtu anayedhibitiwa kwa mbali na mateka wa Waziri Mkuu wa Israel katika vita vya Iran.
-
Muda wa Kuondolewa Vituo vya Kijeshi vya Marekani Barani Ulaya Umeshaanza Rasmi?
May 03, 2026 09:48Wizara ya vita ya Marekani Pentagon imetangaza rasmi kuwa, itawaondoa wanajeshi 5,000 wa nchi hiyo walioko Ujerumani; uamuzi ambao utatekelezwa ndani ya muda wa miezi sita hadi kumi na mbili ijayo.
-
Namna Marekani Ilivyokosa Kuwa na Mkakati Unaoeleweka Katika Kuamiliana na Iran
May 02, 2026 17:20Naibu waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Wendy Sherman, amekosoa namna serikali ya Donald Trump inavyosimamia suala la vita dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa, Washington haina mkakati unaoeleweka, wala mwenendo wa uchukuaji maamuzi ulioratibika, na kwamba mgogoro wa sasa hautatatuka pasi na kuirejea tena diplomasia.
-
Shambulio la Utawala wa Kizayuni Dhidi ya Msafara wa Meli wa Sumud; Mijibizo, Jumbe na Matokeo Yake
May 02, 2026 17:01Wanajeshi wa Kizayuni kwa mara nyingine tena wameushambulia msafara wa Sumud wa meli za kimataifa na kuzuia kupelekwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Mbunge wa Marekani asema Trump ni mtendajinai
May 02, 2026 10:01Mbunge wa chama cha Democratic wa Marekani amemtaja Donald Trump Rais wa nchi hiyo kuwa ni mhalifu mtendajinai.
-
Uchunguzi mpya wa CNN: Kambi nyingi za Marekani Asia Magharibi ziliharibiwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran
May 02, 2026 09:54Uchunguzi mpya wa CNN: Kambi nyingi za Marekani Asia Magharibi ziliharibiwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran
-
Mufti Mkuu wa Russia: Umma wa Kiislamu unapaswa kusimama pamoja na Iran dhidi ya njama za shetani
May 02, 2026 07:35Mufti Mkuu na Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu wa Russia ameeleza kuwa, Umma wa Kiislamu unapaswa kusimama pamoja na Iran dhidi ya njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na akasema: "Iwapo Waislamu watakuwa na umoja na mshikamano, kambi ya shetani haiwezi kamwe kurudia uchokozi dhidi ya Gaza, Syria, Iran na Lebanon."
-
Mbunge wa Kongresi: Ni mwehu anayedai Marekani imeshinda vita dhidi ya Iran
May 02, 2026 07:25Mwakilishi wa cha cha Democratic wa California katika Kongresi ya Marekani, Sara Jacobs, amemkosoa vikali Waziri wa Vita wa nchi hiyo, Pete Hegseth kwa kutangaza ushindi dhidi ya Iran, akitaja madai hayo kuwa ni udanganyifu.