Jumatano, tarehe Mosi Februari, 2017
Leo ni Jumatano tarehe 3 Jamadil Awwal 1438 Hijria 1438 Hijria sawa na tarehe Mosi Februari 2017.
Siku kama ya leo miaka 38 iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo ilikuwa muungaji mkono mkubwa wa utawala wa kidhalimu wa Shah nchini Iran, iliitambua hotuba ya hamasa iliyotolewa na hayati Imam Khomeini MA mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu katika makaburi ya Beheshti Zahra mnamo tarehe 12 Bahman, baada ya kurejea kwake nchini kuwa, ilikuwa dhidi ya Marekani. Katika hotuba hiyo Imam Khomeini alibainisha misimamo yake mkabala wa siasa za kibeberu na uingiliaji wa Marekani katika masuala ya Iran. Kwa upande wake utawala wa Kizayuni wa Israel ulielezea wasiwasi wake kuhusu kurejea Imam Khomeini nchini Iran kwa sababu ulitambua kwamba, Imam na wananchi Waislamu wa Iran ni wapinzani wakubwa wa utawala huo ghasibu na vamizi. Aidha shirika la habari la Russia, Itar-Tass liliripoti kuwa kurejea Ayatullah Ruhullah Khomeini nchini Iran, kumeyafanya mapambano ya wananchi wa nchi hiyo kuingia katika hatua yenye kuainisha mustakbali.
Tarehe Mosi Februari miaka 59 iliyopita iliundwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu baina ya Syria na Misri. Baada ya kumalizika vita vya Suez na kurudi nyuma askari wa Uingereza, Ufaransa na utawala ghasibu wa Israel kutoka katika ardhi ya Misri, Gamal Abdul Nasser alitambuliwa kuwa kiongozi dhidi ya ukoloni wa Magharibi na dhidi ya Uzayuni katika ulimwengu wa Kiarabu na kupata umashuhuri mkubwa. Hatua ya kwanza ya kuanzisha muungano wa nchi za Kiarabu dhidi ya utawala haramu wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi ilichukuliwa tarehe Mosi Februari 1958 baada ya Syria kutia saini makubaliano ya kuungana na Misri na muungano huo ulianza rasmi baada ya kura ya maamuzi ya tarehe 22 Februari 1958 katika nchi hizo mbili. Tarehe Mosi Februari miaka 58 iliyopita iliundwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ya Syria na Misri. Baada ya kumalizika vita vya Suez na kurudi nyuma askari wa Uingereza, Ufaransa na utawala ghasibu wa Israel kutoka katika ardhi ya Misri, Gamal Abdul Nasser alitambuliwa kuwa kiongozi dhidi ya ukoloni wa Magharibi na dhidi ya Uzayuni katika ulimwengu wa Kiarabu na kupata umashuhuri mkubwa. Hatua ya kwanza ya kuanzisha muungano wa nchi za Kiarabu dhidi ya utawala haramu wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi ilichukuliwa tarehe Mosi Februari 1958 baada ya Syria kutia saini makubaliano ya kuungana na Misri na muungano huo ulianza rasmi baada ya kura ya maamuzi ya tarehe 22 Februari 1958 katika nchi hizo mbili.
Siku kama ya leo miaka 203 iliyopita, kulitokea vita vikali na vya umwagaji damu mkubwa maarufu kwa jina la Routier katika eneo lenye jina kama hilo karibu na Mto Ob kati ya jeshi lililokuwa na askari laki moja na 60 elfu la vikosi vya waitifaki wa nchi za Prussia, Austria na Sweden na jeshi lililokuwa na askari elfu 42 la Ufaransa chini ya uongozi wa Napoleon. Katika vita hivyo jeshi la Ufaransa lilishindwa vibaya na waitifaki kutokana na kutokuwa na moyo wa kupigana na uchache wa wapiganaji wake.