Jumapili, 16 Aprili, 2017
Leo ni Jumapili tarehe 18 Rajab 1438 Hijiria, mwafaka na tarehe 16 April, 2017 Miladia.
Leo ni Jumapili tarehe 18 Rajab 1438 Hijiria, mwafaka na tarehe 16 April, 2017 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 2482 iliyopita, yaani sawa na tarehe 16 April mwaka 465 kabla ya kuzaliwa Nabii lssa (as) na kwa mujibu wa mahesabu, uoanishaji wa takwimu na vyanzo vya habari, mji wa Takht-e-Jamshid (Shiraz) ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Iran. Ardashir wa Kwanza ambaye alichukuwa nafasi ya baba yake na kuwa mfalme wa Iran, katikati ya mwezi Aprili mwaka 465 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa aliamua kuutangaza mji huo kuwa mji mkuu wa kwanza wa Iran (na makao makuu ya mfalme.) Baadaye wanahistoria wa Ugiriki waliutawambua mji wa Takht-e-Jamshid kwa jina la Persepolis. Siku ulipotangazwa mji wa Takht-e-Jamshid kuwa mji mkuu wa Iran, mji wa Shush pia ulitangazwa kuwa makao makuu ya kiofisi kwa ajili ya shughuli za serikali, ambapo katika msimu wa joto, wafanyakazi wa serikali waliweza kufunga safari na kwenda mjini Hamadan kwa ajili ya kutekekeleza wadhifa wao wa kiserikali. Ni kwa ajili hiyo ndio maana wataalamu wa historia wa Ugiriki wakaifahamu Iran ya enzi za utawala wa Achaemenid, kuwa iliyokuwa na miji mikuu mitatu.
Siku kama ya leo miaka 1428 iliyopita, alifariki dunia mtoto mdogo wa Mtume wetu Muhammad (saw), Ibrahim akiwa na umri wa miezi 18 tu. Ibrahim ambaye alifariki dunia kutokana na maradhi, alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa Mtume ambaye hakuzaliwa na Bibi Khadija (as). Mama yake alikuwa Maria al Qibtiyya ambaye alitumwa na mfalme wa Misri ya wakati huo kuwa hadimu na mtumishi wa Mtume na aliolewa na mtukufu huyo baada ya kusilimu. Kifo cha Ibrahim kilimhuzunisha sana Mtume (saw) kwa sababu mtukufu huyo alikuwa akimpenda sana.
Tarehe 18 Rajab miaka 1012 iliyopita alifariki dunia Ibn Samh huko Andalucia. Msomi huyo wa Kiislamu alikuwa mtaalamu wa hesabu, nyota na tabibu. Alizaliwa katika mji wa Cordoba, Andalucia mnamo mwaka 370 Hijiria. Msomi huyu wa Kiislamu alifanya utalii na utafiti mwingi katika elimu za hesabu na nyota, sambamba na kuwalea wanafunzi wa zama zake. Kuna vitabu kadhaa vilivyoandikwa na Ibn Samh kwa lugha ya Kiarabu na miongoni mwavyo ni pamoja na kitabu kiitwacho "Al Madkhalu Ila al Handasah", "Al Muamalat" na "Kitabuz Zaij."
Siku kama ya leo miaka 218 iliyopita alizaliwa huko kaskazini mwa Iran, Allamah Haj Mula Muhammad, maarufu kwa jina la Hujjatul-Islami Ashrafi, alimu mkubwa wa Waislamu. Ili kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu alifanya safari mjini Najaf, Iraq na kusoma kwa maulama wakubwa wa zama hizo. Baada ya muda mfupi Allamah Haj Mula Muhammad alitokea kuwa msomi mkubwa katika elimu ya hadithi, tafsiri ya Qur’ani na theolojia. Hujjatul-Islami Ashrafi alifariki duni mwaka 1315 Hijiria. Ameandika vitabu vingi vyenye thamani kubwa baadhi vikiwa vimepotea. Kitabu maarufu ni kile kinachoitwa ‘Asraaru sh-Shahaadah.’
Siku kama ya leo miaka 173 iliyopita, alizaliwa Anatole France, mwandishi na malenga wa Ufaransa. Akiwa kijana alipendelea sana kujifunza fasihi na uandishi na harakaharaka akapata umashuhuri mkubwa kutokana na kwamba alikuwa na maandalizi makubwa katika uwanja huo. Ameandika vitabu vingi kikiwemo kitabu alichokipa jina la ‘Jumba la Konokono’ na ‘Malikia wa Sabai (Sheba).’ Mwaka 1914 Anatole France alipata tuzo ya Nobel kutokana na kuandika kitabu alichokiita ‘Uasi wa Malaika.’ Anatole France alifariki dunia mwaka 1924 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 158 iliyopita alifariki dunia Alexis de Tocqueville, mwandishi na mwanasosholojia wa nchini Ufaransa. Alizaliwa mwaka 1805 ambapo akiwa kijana alisomea elimu ya falsafa na sheria. Kama alivyokuwa baba yake, Tocqueville alifanya juhudi za kuingia serikalini na baadaye akawa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo. Aidha kuanzia mwaka 1959 alikuwa mbunge wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 12. Mbali na masuala ya kisiasa, Tocqueville alianza kufanya utafiti wa masuala ya jamii na hivyo akafanya safari katika mataifa mbalimbali kama vile, Italia, Ujerumani, Uingereza na Marekani. Ameandika vitabu vingi vikiwemo vya ‘Utawala wa zamani na Mapinduzi ya Ufaransa’ na ‘Demokrasia nchini Marekani.’
Siku kama ya leo miaka 128 iliyopita, Charles Spencer Chaplin mcheza filamu na msanii mashuhuri wa tasnia ya filamu alizaliwa katika viunga vya mji wa London Uingereza. Alipokuwa mdogo, alianza kujishughulisha na michezo ya kuigiza na kupata umashuhuri hatua kwa hatua. Mwanzoni mwa ujana wake, Chaplin alielekea nchini Marekani kwa lengo la kutengeneza filamu. Lakini kutokana na kutengeneza filamu za ukosoaji na zenye kuonyesha mshikamano wake na matabaka ya kimasikini katika jamii ya Marekani, serikali ya nchi hiyo ilitoa amri ya kubaidishwa kwake mnamo mwaka 1952. Chaplin alikumbana na mazingira magumu ya kufanya shughuli zake nchini Marekani na hivyo akahamia nchini Uswisi pamoja na mkewe. Msanii huyo katika tasnia ya filamu alifariki dunia mwaka 1977.
Siku kama ya leo miaka 128 iliyopita, Charles Spencer Chaplin mcheza filamu na msanii mashuhuri wa tasnia ya filamu alizaliwa katika viunga vya mji wa London Uingereza. Alipokuwa mdogo, alianza kujishughulisha na michezo ya kuigiza na kupata umashuhuri hatua kwa hatua. Mwanzoni mwa ujana wake, Chaplin alielekea nchini Marekani kwa lengo la kutengeneza filamu. Lakini kutokana na kutengeneza filamu za ukosoaji na zenye kuonyesha mshikamano wake na matabaka ya kimasikini katika jamii ya Marekani, serikali ya nchi hiyo ilitoa amri ya kubaidishwa kwake mnamo mwaka 1952. Chaplin alikumbana na mazingira magumu ya kufanya shughuli zake nchini Marekani na hivyo akahamia nchini Uswisi pamoja na mkewe. Msanii huyo katika tasnia ya filamu alifariki dunia mwaka 1977.
Na siku kama ya leo miaka 20 iliyopita ulitokea mlipuko mkubwa ulisababishwa na mtungi wa gesi na kusambaza moto kwenye mahema ya Mahujaji huko Mina kilomita 10 kutoka katika mji Mtakatifu wa Makka. Mahujaji wasiopungua 343 walifariki dunia na wengine 1,290 kujeruhiwa katika tukio hilo chungu. Aidha mahema yasiyopungua elfu sabini yaliteketea kwa moto huo. Hilo linahesabiwa kuwa tukio kubwa la pili la janga la moto kutokea wakati wa msimu wa Hija. Mnamo mwaka 1975, ulitokea moto mkubwa huko Mina nchini Saudi Arabia uliosababisha vifo vya maelfu ya Mahujaji na wengine wengi kujeruhiwa. Kutokana na matukio hayo, Saudi Arabia ililazimika kuweka katika eneo la Mina, mahema yasiyoshika moto ili kuepusha ajali za moto.