Uungaji Mkono wa Marekani kwa Israel; Sababu na Kwa Nini
Hamjambo wapendwa wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi katika kipindi chetu cha makala ya wiki, ambapo juma hili tutazungumzia uungaji mkono wa Marekani kwa Israel, sababu na kwa nini. Karibuni.
Israel ni kambi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, na ni chanzo cha migawanyiko na mikwaruzano na kukandamizwa harakati za ukombozi.
Sera za nje za Marekani katika miaka iliyopita zilijengeka katika kuunga mkono kwa pande zote maslahi ya Israel katika eneo la Asia Magharibi na katika ngazi ya mfumo wa kimataifa. Nchi hiyo ni kati ya nchi ambazo katika miaka kadhaa ya karibuni zimekuwa zikiunga mkono jinai za Wazayuni na utawala wa Kizayuni pia umeendeleza jinai zake za kinyama kwa miaka hiyo yote kwa uungaji mkono huo wa Magharibi na Marekani. Marekani haina mipaka katika kutoa msaada mkubwa wa kifedha na kijeshi kwa utawala bandia wa Israel, na wala haiuainishii masharti yoyote utawala huo ghasibu. Moja ya mambo yaliyobainika zaidi hivi karibuni na taswira ya Marekani ambayo siku zote inadai kutetea haki za binadamu na huku ikitoa madai hayo ya uwongo inazishinikiza nchi nyingine huru duniani ni kwamba walimwengu wametambua kuwa uungaji mkono wa nchi hiyo kwa utawala bandia wa Israel katika kuwauwa watoto, wanawake na raia wa Palestina huko Ghaza hauishihi tu katika maidani bali tunashuhudia Marekani katika diplomasia na ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia likiyapigia kura ya veto maazimio yanayotaka kutekelezwa usitishwaji vita Ukanda wa Ghaza ili kuwezesha kutumwa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa eneo hilo.

Swali hili linaulizwa kwamba, uungaji mkono huu mkubwa unaotekelezwa kwa kusaidiwa na kupatiwa misaada ya pande zote ya kidiplomasia na vyombo vya habari unatekelezwa kwa mantiki na malengo gani?
Chunguzi zinaonyesha kuwa lobi ya Wazayuni wenye ushawishi huko Marekani wako nyuma na uungaji mkono na misaada hiyo isiyo na masharti kwa Israel. Ushawishi wa Israel nchini Marekani ni mojawapo ya mifano ya kipekee ya ushawishi na satwa iliyonayo Israel katika sera za ndani na nje ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, karibu zaidi ya asilimia 90 ya Wayahudi wa Marekani wanashiriki katika uchaguzi wa nchi hiyo na wana mchango na kuathiri pakubwa matokeo ya uchaguzi.
Noam Chomsky Mwanafalsafa na mwanaisimu mtajika wa Marekani anaashiria namna fedha zilivyo na taathira katika uchaguzi wa Marekani na kusema:" Matokeo ya uchaguzi wa Marekani yanaweza kutabiriwa kwa kiwango na kiasi cha fedha kinachotumika katika uchaguzi; na huathiri moja kwa moja mchakato huo kwa kuwa makundi ya Kiyahudi na hasa Wazayuni ambao wanafadhili fedha nyingi ili kusaidia mchakato wa uchaguzi ni miongoni mwa wagombea.

Wakati huo huo makundi hayo yana nafasi muhimu sana katika nyanja mbalimbali ndani ya jamii ya Marekani na hasa katika uga wa siasa na vyombo vya habari. Vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na Wazayuni vina mchango mkubwa katika kubadili fikra za waliowengi na au kumuarifisha mgombea fulani; na kwa msingi huo kwa kutambua kiwango na nguvu ya ushawishi wa kundi hilo la wachache kwa vyombo vya habari, wagombea wa kiti cha urais nchini Marekani wanajaribu kwenda sambamba na matakwa ya Wayahudi na hivyo waweze kujipatia kura nyingi kupitia kuungwa mkono na vyombo hivyo vya habari.
Lobi ya Wazayuni yenye ushawishi mkubwa ya AIPAC ndiyo inayogharamia moja kwa moja kampeni za wawakilishi wa Kongresi ya Marekani na safari zao katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kuimarisha uhusiano baina yao na viongozi na maafisa wa jamii ya Kizayuni.
Imeelezwa kuwa, kamati hiyo ina wajumbe karibu elfu sitini kote nchini Marekani na inafanya kazi kwa maslahi ya Israel, na kila mwaka huingiza kiasi kikubwa cha fedha kwenye akaunti za Lobi ya Wazayuni katika benki zilizoko Marekani. Kamati hiyo ina taathira kubwa miongoni mwa fikra za waliowengi na hushiriki katika maamuzi ya serikali.
Hivi ndivyo Lobi ya Wazayuni inavyoanzisha uhusiano imara na mpana na maafisa wa ngazi za juu wa kisiasa nchini Marekani. Kwa mfano, katika miaka ya 1994 na 1996 wajumbe wa AIPAC walikutana karibu na wagombea 6000 wa uchaguzi wa Kongresi ya Marekani.

Lobi hiyo ya Wayahudi ambayo ina historia ndefu sana katika ushiriki wake kisiasa huko Marekani imeundwa na makundi mawili makubwa ya Wayahudi Wazayuni; ambapo shakhsia wake wenye ushawishi wanashikilia nyadhifa mbalimbali, ikiwemo uwepo wao katika taasisi za uchukuaji maamuzi za Marekani huku wakiwa na mchango na ushawishi mkubwa katika sera za nje za nchi hiyo. Viongozi muhimu sana wa kisiasa wa Marekani kama Martin Indyk Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa zamani wa Marekani katika Masuala ya Mashariki ya Karibu, na Dennis B.Ross Mratibu wa zamani wa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati na Mel Sembler Mwenyekiti wa Idara ya Fedha ya Kamti ya Taifa ya chama cha Republican ni miongoni mwa wajumbe wa kundi hilo.
Kwa msingi huo, katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita na hasa tangu kujiri vita vya siku sita mwaka 1967, sera za Marekani zimekuwa zikitoa uzito na kipaumbele kwa suala la kuwa na uhusiano na utawala wa Israel.
Wakati huo huo uungaji mkono usio na kikomo wala kigugumizi wa Marekani kwa utawala ghasibu wa Israel na kigugumizi kwa Israel na madai yake ya uwongo ya kukuza "demokrasia" katika eneo lote la Mashariki ya Kati vimeibua hasira na ghadhabu za jamii ya Waarabu na Ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya siasa ghalati na ulaghai za Marekani za kuunga mkono utawala haramu wa Kizayuni. .
Katika historia ya sera za nje za Marekani, makundi yote yenye maslahi maalum yameibua ukinzani katika sera za nje za nchi hiyo, hata hivyo hakuna kundi lolote lenye ushawishi kama Lobi ya Wazayuni ambalo limeweza kuiaminisha serikali na wananchi wa Marekani kwamba maslahi ya nchi hiyo na Israel yanashabihiana kikamilifu.
Tangu kujiri vita vya Oktoba mwaka 1973, Washington imeiunga mkono pakubwa Israel kulinganisha na nchi nyingine. Tokea mwaka 1976, uungaji mkono huo unajumuisha kutolewa kila mwaka misaada mikubwa na ya moja kwa moja ya kiuchumi na kijeshi; misaada mbayo inatajwa kuwa mikubwa zaidi kuwahi kutolewa na Marekani kwa serikali nyingine tangu kujiri Vita vya Pili vya Dunia ambapo misaada hiyo kwa urahisi kabisa imefikia thamani ya dola bilioni 140.
Katika fremu ya uungaji mkono wa Marekani na kwa mujibu wa baadhi ya takwimu zilizopo, Israel kila mwaka hupokea msaada wa moja kwa moja wa karibu dola bilioni tatu, ambao takriban unajumuisha moja ya tano ya bajeti ya misaada ya nje na thamani yake inakadiriwa kuwa karibu dola 500 kwa kila mtu raia mmoja wa utawala wa Israel. Nukta nyingine ya kuzingatia ni kuwa, nchi nyingine zinazopokea misaada kutoka Marekani hupata misaada hiyo kwa awamu kila baada ya miezi mitatu hata hivyo israel hupatiwa misaada yote na Marekani kwa pamoja mwanzoni mwa mwaka mpya wa fedha; na kwa utaratibu huo Israel inaweza kunufaika pakubwa kutokana na misaada hiyo. Aidha ni vyema kuzingatia kuwa, wapokeaji wengi wa misaada ya kijeshi wanatakiwa kutumia huko Marekani fedha zote wanazopokea lakini Israel inaruhusiwa kutoa ruzuku ya karibu asilimia 25 ya misaada hiyo katika sekta yake ya ulinzi. Wakati huo huo Israel ni utawala pekee unaopata misaada ya kijeshi kutoka Marekani ambako hakuna ulazima wa kuieleza kuhusu namna ya kutumia misaada hiyo, na pia Israel ndiyo inayopokea misaada ya kijeshi kutoka Marekani pekee ambayo hailazimiki kuieleza nchi hii jinsi inavyotumika, na hii inasababisha kushindwa kuzuiwa matumizi ya fedha hizo katika masuala ambayo yanaonekana kupingwa na Marekani kama vile ujenzi wa vitongoji katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Mbali na haya, Marekani huipatia pia Israel misaada mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza mifumo ya silaha ya utawala huo na hivyo kuuandalia uwanja utawala huo wa kumiliki silaha za kisasa zaidi kama helikopta aina ya Black Hawk na ndege za kivita za F-16.
Kwa mujibu wa makubaliano ya pande mbili kati ya Marekani na utawala wa Kizayuni, ya mwaka 2016, iliamuliwa kuwa Marekani katika kipindi cha mwaka 2019 hadi 2028 itatumia dola bilioni 33 kugharamia zana za kijeshi huko Israel.
Ni jambo la kushangaza pia ikiwa tunajua kuwa Amerika haisiti kuwapa Israel habari za kijasusi, ambazo pia inakataa kuwapa washirika wake katika NATO huku ikifumbia macho pia juhudi za Israel za kumiliki silaha za nyuklia. Mbali na uungaji mkono huo wa kimaidani, Marekani ni muungaji mkono mkuu wa utawala wa Kizayuni katika uga wa diplomasia kwa kadiri kwamba tangu mwaka 1982 hadi kabla ya kuanza Kimbunga cha Al Aqsa, Marekani imeyapigia kura ya turufu maazimio yasiyopungua 32 ya Baraza la Usalama yaliyoilaani Israel; na idadi hii ni zaidi ya jumla ya kura za turufu zilizowahi kupigwa na nchi nyingine wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Marekani siku zote imekuwa ikiegemea upande wa utawala wa Kizayuni hata wakati wa kufikiwa makubaliano ya amani huku ikipasa kuwa msuluhishi. Kwa mfano, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki katika mazungumzo ya Camp David mwaka 2000 ameeleza kuwa: Mara nyingi tulikuwa tukichukua hatua kama wakili wa Israel."
Nukta ya mwisho ni kuwa, inaonekana kuwa pamoja na ushawishi mkubwa wa Lobi ya Wayahudi wenye nguvu huko Marekani, kuna maslahi muhimu na ya kistratijia kwa Marekani katika uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni, na maslahi haya muhimu na ya kistratejia ndiyo yanayopelekea kusalia na kuendelea kwa donda hili la saratani. Ni wazi kuwa lengo kuu la uungaji huu mkono usio wa kawaida kwanza kabisa, unatokana na maslahi ya kistratijia ya Marekani, maslahi ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusiana na nafasi kuu na maalumu ya utawala huo katika stratejia ya Marekani; na kwa mujibu wake, Israel inahesabiwa kama kambi ya kijeshi ya Marekani katika Mashariki ya Kati ambayo ni chanzo cha migawanyiko na au kuzikandamiza harakati za ukombozi katika eneo. Kama alivyokiri Mzayuni mmoja, Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni ngome ya Marekani; na Israel haipigani kwa ajili ya kujilinda tu, bali pia inapigana kwa ajili ya maslahi muhimu ya nchi za Magharibi.