Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Watoto Katika Nchi za Magharibi
Jamii za Wamagharibi, khususan zile zilizoendelea na zinazodai kutetea ubinadamu za Ulaya, zina sura nyingine isiyoonekana waziwazi kwa watu wengi.
Sura hiyo ya upande wa pili ya nchi za Magharibi hufichuliwa na kuwekwa wazi katika nyakati makhsusi, lakini juhudi kubwa hufanyika haraka ili sura hiyo isahauliwe na walimwengu. Idara ya Polisi ya Makosa ya Jinai ya Shirikisho la Ujerumani imetahadharisha katika ripoti yake ya karibuni kuhusu uhalifu wa kijinsia na udhalilishaji wa kingono wanaofanyiwa watoto na mabarobaro ikisema kwamba mwaka uliopita wa 2022 watoto zaidi ya elfu 17 walio na umri wa chini ya miaka 14 walikuwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini humo. Polisi ya Ujerumani imetangaza katika ripoti hiyo kwamba, ksi ambazo hazikuripotiwa za uhalifu huo zinaweza kuwa mara kadhaa ya takwimu zilizopo. Kwa mujibu wa ripoti ya Dutch Welle, karibu robo ya vitendo vya ukatili huo wa udhalilidhaji kingono ilitokea mwaka jana wa 2022 katika jimbo la North Rhine-Westphalia huko Ujerumani lenye jamii ya watu karibu milioni 18. Katika upande mwingine, suala la kuenea kwa ponografia dhidi ya watoto na mabarobaro limetajwa katika ripoti ya mwaka jana ya Idara ya Polisi ya Jinai ya Shirikisho la Ujerumani; ambapo uhalifu unaohusiana na kadhia hii umeongezeka kwa asilimia 7.5 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake na kufikia kesi 42,000.
Nancy Faeser, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, anasema: Ripoti hiyo inaonyesha wazi kiwango cha kutisha cha ukatili wa kingono dhidi ya watoto nchini humo. Serikali ya Ujerumani kwa miaka kadhaa sasa inajiarifisha kama mtetezi wa haki za watoto na inayopamba dhidi ya mateso na udhalilishaji wa watoto; hata hivyo hali wanayopitia watoto na mabarobaro katika nyanja mbalimbali inaekelea kuwa mbaya sana. Hali hii mbaya imepelekea kuanzishwa Ofisi ya Kamishenia Huru ya Kufuatilia Vitendo vya Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watoto mwaka 2010 ambapo sheria za uhalifu zimeimarishwa kwa kiasi kikubwa katika uwanja huo. Hata hivyo hadi sasa hakuna ishara inayoonyesha kuboreka kwa hali ya mambo. Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Afya Duniani (WHO), watoto na mabarobaro zaidi ya milioni moja huko Ujerumani mwaka jana walifanyiwa ukatili wa kingono na watu wazima. Kiwango hiki kina maana ya ukatili wa kingono dhidi ya mtoto mmoja au wawili katika kila darasa la shule nchini Ujerumani. Ripoti ya WHO imebainisha kuwa, kesi nyingi kati ya hizi hazijajumuishwa katika takwimu za uhalifu kwa sababu kamwe haziripotiwi na hazipewi uzito na kutiliwa maanani.
Ukatili na unyanyasaji wa kingono kwa watoto na mabarobaro nchini Ujerumani katika miaka ya karibuni limekua tatizo linalokua siku baada ya siku ambalo inashindakana kudhibitiwa. Takwimu za taasisi rasmi za serikali ya Ujerumani zinaeleza kuwa, hali hii ni mbaya na yenye kutia wasiwasi kwa mabarobaro na watoto wa Ujerumani. Unyanyasaji huu wa watoto hauko Ujerumani pekee, bali katika nchi nyingi za Ulaya pia unyanyasaji wa kingono kwa watoto limekuwa jambo la kawaida. Kiasi kwamba serikali ya Ufaransa imepunguza umri wa maingiliano ya kingono na mabarobaro ili eti kwamba watu wengi waondolewe kwenye orodha ya uhalifu wa mahusiano na mabarobaro. Nukta ya kupewa mazingatio hapa ni kuwa, Ufaransa imepunguza umri wa kujamiiana na vijana kwa kisingizio cha kupiga vita ukatili wa kingono! Sheria mpya ya nchi hiyo inaeleza kuwa, mtu mzima akijamiiana na mtoto aliye chini ya umri wa miaka 15 au na jamaa yake wa karibu aliye chini ya umri wa miaka 18 vinahesabiwa kuwa ndio ubakaji.
Takwimu zilizotangazwa kuhusu kuongezeka unyanyasaji kwa watoto katika nchi za Magharibi zinaonyesha kuporomoka thamani na maadili ya kibinadamu. Nukta muhimu kuhusu kuporomoka thamani za kiakhlaqi na kibinadamu ni kwamba taasisi za kidini, kama kanisa, ambazo zinapasa kukuza maadili mema zinabeba dhima ya suala hili la kuporomoka thamani za kiakhlaqi na kibinadamu. Katika miaka ya karibuni Kanisa Katoliki limekumbwa na kashfa ya mapadri wanaowadhalilisha watoto kingono. Papa, Kiongozi wa Wakatoliki Duniani, kila anapofanya ziara maeneo na nchii mbalimbali duniani hasa katika nchi zenye wafuasi wa Kanisa Katoliki, analazimika kuomba radhi kwa vitendo na tabia za mbaya za mapadri za kuwadhalilisha kingono watoto wadogo. Uchunguzi wa maoni ulioshirikisha zaidi ya watu elfu 8 umeonyesha kuwa asilimia 6 ya idadi ya watu milioni 39 nchini Uhispania walisema walinyanyaswa kingono na makasisi katika kiipindi cha utotoni mwao.
Angel Gabilondo, Waziri wa zamani wa Elimu wa Uhispania anasema kuhusu suala hilo kwamba: "Kwa bahati mbaya, kwa miaka kadhaa sasa juhudi zimefanywa ili kuwalinda wahalifu hao wanyanyasaji au kuzuia kuchapishwa taarifa zinazowahusu. Gazeti la El Pais kwa upande wake limeandika kuwa: "Hii ni ncha tu ya kilelea cha mlima wa barafu." Kamisheni moja inayojitegemea nchini Ufaransa pia mwaka 2021 ilifikia hitimisho kwamba, kuanzia mwaka 1950 watoto wapatao laki 2 na elfu 16, wengi wao wakiwa wavulana, walinyanyaswa kingono na makasisi. Huko Ujerumani pia matokeo ya utafiti uliofanywa nchini humo yameonyesha kuwa, visa 3,677 vya udhalilishaji wa kingono vimefanywa na makasisi wa Kanisa Katoliki kati ya mwaka 1946 hadi 2014. Wakati kashfa na uhalifu mkubwa wa ukatili wa kingono kama huu unaporipotiwa makanisa, inabainika kwamba, tatizo hilo ni kubwa kupita kiasi katika matabaka mengine ya jamii za Wamagharibi.
Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Polisi ya Uhispania, kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu; mmoja kati ya wahalifu wanane wa ukatilii wa kingono waliokamatwa Kaskazini Mashariki mwa Uhispania alikuwa mtoto mdogo. Data zilizopo zinaonyesha kuwa hali ni mbaya sana kwa watoto na vijana; ambapo tabaka hili sio tu kwamba wao ni waathirika wa mgogoro wa ukatili wa kingono unaoongezeka kwa kasi, lakini pia ni sehemu ya wahalifu wa vitendo vya udhalilishaji kingono.
Nchi za Magharibi zimepiga hatua na kupata maendeleo katika nyanja za sayansi na uchumi na kuboresha maisha ya kimaada ya watu, lakini kwa kadiri hiyo hiyo pia, zimejiweka mbali na thamani za kimaadili na maumbile asili ya mwanadamu. Nchi hizo zinafundisha mahusiano haramu ya ngono baina ya watoto na vijana kwa kutuumia jina la kuwakinga na madhara ya kijamii. Mafunzo haya na kuporomoka kwa thamani za familia huwa msingi wa kuporomoka kimaadili kati ya mabarobaro na vijana. Kwa jina la uhuru na usawa kati ya wanawake na wanaume, wanawake wamekuwa bidhaa ya kukidhi matamanio ya ngono ya wanaume, na ukahaba umekuwa tasnia ya kuingiza mapato ya taifa.
Wakati huo huo nchi za Magharibi zimeutambua rasmi ushoga unaopingana na maadili na maumbile asili ya binadamu kwa kisingizio cha kuheshimu haki za walio wachache. Takwimu rasmi zilizochapishwa na serikali za nchi za Magharibi zinaonyesha janga na kuenea pakubwa vitendo vya ukahaba na kuporomoka thamani za kimaadili katika nchi hizo. Marekani ambayo ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, mwaka uliopita ilipatia dola bilioni 14.6 kutokana na sekta hii ya ukahaba. Ni wazi kuwa faida inayopatikana kutokana na sekta ya ukahaba nchini Marekani ni kubwa zaidi ya faida jumla ya makampuni yote ya teknolojia ikiwa ni pamoja na Google, Netflix, Apple, Amazon, eBay, Microsoft, EarthLink na Yahoo.
Katika nchi nyingine za Magharibi pia ukahaba na utumwa wa ngono kwa wanawake ni tasnia inayozalisha pesa, na serikali pia hukusanya ushuru kutoka kwenye madanguro hayo. Katika uchunguzi wa historia na kuporomoka staarabu mbalimbali tunaona kuwa, moja ya sababu za kuanguka ustaarabu na tawala kubwa ni kuporomoka kwa maadili, na kushamiri matendo yaliyo kinyume na maumbile ya mwanadamu.
Kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, Qur'ani Tukufu, pia kimetaja mifano kadhaa ya visa hivi vilivyopelekea kuangamizwa umma zilizopita na kutoweka staarabu za mataifa hayo.