Watanzania waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10378-watanzania_waadhimisha_siku_ya_kimataifa_ya_quds
Wananchi wa Tanzania wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds hii leo ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni katika kuonyesha mshikamano wao na muqawama wa wananchi wa Palestina mbele ya maghasibu Wazayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 01, 2016 10:57 UTC
  • Watanzania waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds

Wananchi wa Tanzania wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds hii leo ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni katika kuonyesha mshikamano wao na muqawama wa wananchi wa Palestina mbele ya maghasibu Wazayuni.

Wananchi wa Tanzania leo Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani wameungana na Waislamu wenzao wa nchi nyingine kwa kushiriki kwenye maandamano jijini Dar es Salaam ambapo wamesisitiza kuendeleza umoja na mshikamano wao na kuunga mkono mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina walio chini ya ukandamizaji wa Wazayuni maghasibu.

Ripoti kutoka Dar es Salaam zinasema kuwa kesho Jumamosi kutafanyika semina ya Quds jijini Dar es Salaam iliyoitishwa na kamati ya Mshikamano ya Palestina na Tanzania. Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu, Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhanii kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds; ambapo katika siku hiyo kila mwaka Waislamu kote ulimwenguni hujitokeza mitaani kufanya maandamano ya kulaani jinai za Wazayuni na kutangaza mshikamano wao kwa wananchi madhlumu wa Palestina.

Huko Nigeria pia Waislamu nchini humo wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds bila ya kuwepo kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye anashikiliwa katika jela nchini humo. Waislamu katika maandamano ya leo ya Quds walidhihirisha hasira zao kwa utawala wa Kizayuni unaotefanya mauaji ya watoto huko Palestina. Waislamu wa Nigeria pia walibeba mabango yenye picha za kiongozi wao Sheikh Ibrahim Zakzaky na za watoto wake waliouliwa shahidi na kutangaza uungaji mkono wao kwa kiongozi huyo. Wananchi wa nchi mbalimbali pia wameshiriki kwenye maandamano ya leo ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika kuitetea Quds Tukufu na kuonyesha mshikamano wao kwa wananchi wa Palestina.