Nchi zisizo za Kiislamu zatakiwa kuheshimu haki za Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10495-nchi_zisizo_za_kiislamu_zatakiwa_kuheshimu_haki_za_waislamu
Mshauri iwa Rais wa Misri amesema kuwa upo ulazima kwa nchi zisizo za Kiislamu kuheshimu haki za Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 03, 2016 08:51 UTC
  • Nchi zisizo za Kiislamu zatakiwa kuheshimu haki za Waislamu

Mshauri iwa Rais wa Misri amesema kuwa upo ulazima kwa nchi zisizo za Kiislamu kuheshimu haki za Waislamu.

Sheikh Usama al Azhari Mshauri wa Rais wa Misri amesema kuwa nchi zisizo za Kiislamu zinapasa kuheshimu haki za Waislamu kama walivyo wanadamu wengine. Sheikh Usama al Azhari ameongeza kuwa Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu wanalinda utambulisho wa dini yao na kwamba serikali mbalimbali zinapasa pia kuheshimu haki za Waislamu.

Mshauri wa Rais wa Misri amelaani mapigano yoyote na hitilafu baina ya Waislamu na kubainisha kuwa siasa zinazotekelezwa na Chuo Kikuu cha al Azhar huko Misri zinaunga mkono fikra za Kiislamu kwa minajili ya kuwasaidia Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu. Sheikh Usama al Azhari amesema kuwa Waislamu milioni 450 wanaishi katika nchi zisizo za Kiislamu. Itakumbukwa kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu (OIC) mwaka 1998 iliasisi jopo kazi kwa minajili ya kupigania na kulinda haki za Waislamu wanaoishi katika nchi zisizo za Kiislamu.